****************************
Mbunge Jimbo la Bumbuli Mkoani Tanga January Makamba amesema kuwa atahakikisha vijiji na vitongoji vya halmashauri hiyo ambavyo havijafikiwa na umeme vinafikiwa ili viweze kuondokana na changamoto ya giza
Akizungumza katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo Makamba alisema wakati anaingia madarakani alikuta ni kata nne tu ndo zilikuwa na huduma ya umeme lakini hivi Sasa kata 15 Kati ya 18 tayari zimeshafikiwa na huduma hiyo.
Alitaja kata tatu ambazo hazina umeme kabisa kuwa ni Milingano ,Kwemkomole na Kisiwani.
Mbunge huyo alisema kuwa alipoingia madarakani aliahidi kupeleka umeme kila Kijiji na ahadi hiyo ameitimiza kwa kiasi kikubwa na Sasa anapigania kata zilizobaki zinapate ili awamu nyingine aanze na vitongoji vyote katika Jimbo la bumbuli.
” Kama umeme huu ungekuwa haujafika kabisa arafu Mbunge akaahidi kupeleka kwenye vitongoji basi ujue huyo ni tapeli naomba muendelee kusubiri umeme utafika kwani maendeleo yakipatikana ata Mimi mbunge nafurahi”Alisema Makamba.
Makamba alisisitiza kuwa ilani ya chama cha mapinduzi CCM inaelekeza kuwa
maeneo yote ambayo hayajafikiwa na umeme yafikiwe ili wananchi wa maeneo husika waweze kuondokana na giza na wakae kwenye mwanga.
Alisema kuwa dalili yakwamba umeme utafika maeneo yote tayari
baadhi ya nguzo zinaoneka tofauti na miaka ya nyuma iliyopita hakukuwa na
nguzo hata moja hivyo endeleeni kuwa na uvumili ili tuweze kumalizia changamoto zilizopo na ahadi zake.
Mbali na umeme Makamba aliahidi uboreshaji wa miundombinu mingine ikiwemo uboreshaji wa shule za msingi na sekondari katika awamu hii
lengo likiwa ni kuweka mazingira bora ya kujifunzia wanafunzi ili kuwapa hamasa ya kuongeza ufaulu katika masomo yao.
Alisema kwenye elimu kunachangamoto kubwa sana na kila shule inaupungufu furani wa kitu na hili ni tatizo la nchi nzima na changamoto hiyo inapelekea ufaulu duni.
Wananchi wa Jimbo hilo wamempongeza Mbunge huyo kwa Kuendelea kuwasaidia katika suala zima la maendeleo hivyo wanaamini Mbunge wao kwa kushirikina na serikali umeme utafika kila mahali na ahadi alizoahidi za kumaliza changamoto zinakamilika.