************
NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO
Agost 4
MBUNGE wa viti Maalumu Mkoani Pwani Zaynab Vullu, amekabidhi kitanda ,baadhi ya vifaa vya vinavyotumika wakati wa kujifungua (delivery kit) pamoja na pempas za watu wazima, katika zahanati ya kijiji cha Yombo ,jimbo la Bagamoyo .
Akiambatana na mwenyeji wake mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa, Zainab alisema hatua hiyo inalenga kusaidia akinamama wanaokwenda kujifungua na wakazi wa kata hiyo kijumla.
Alisema, akishirikiana na wabunge wenzake wa majimbo wamekuwa na ushirikiano katika kusaidia na kupambana na changamoto zinazowakabili wananchi kwenye sekymta mbalimbali ikiwemo afya.
“Nimekuja katika zahanati hii kwa ajili ya kukabidhi kitanda hiki kitachotumika kwa wagonjwa tunaopata huduma hii hapa,pamoja na vifaa vingine na pempas za watu wazima,” alisema Vullu.
Nae Dkt. Kawambwa alimshukuru Zaynab kwa mapenzi aliyoyaonesha kwa wana-Yombo, kufuatia kukabidhi kitanda, godoro pamoja na mifuko yenye vifaa maalumu vya kuwasitiri wagonjwa wa kike na kiume wakati wanapatiwa huduma.
Alisema ,vifaa hivyo vitawasaidia wagonjwa watakaohitaji huduma hizo,na amewaomba wadau wa sekta hiyo kuendelea kuiangalia sekta hiyo ili kuiunga mkono serikali.
Kwa upande wake muuguzi wa zamu Anna Mzeru alibainisha ,vifaa vilivyotolewa na mbunge huyo vina uwezo wa kuwahudumia wagonjwa watano.
Wakati huo huo ,wakazi wa Kijiji cha Yombo Kata ya Yombo jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wanatamani kubadilishana kopo la korosho na kilo ya unga, ili kujikimu kimaisha kutokana na kukabiliwa na hali mbaya kiuchumi.
Hali hiyo imetokana na kutegemea kilimo cha korosho na mahindi, huku sekta hiyo ikikabiliwa na changamoto luluki, iliwemo kuchelewa malipo ya korosho na mifugo kula mazao yao mashambani..
Mkazi mzee Makorosho, akiwakilisha wenzake katika mkutano ulioitishwa na Mbunge Dkt. Shukuru Kawambwa, alieleza, kucheleweshwa malipo ya korosho wanaishi maisha magumu, huku wakitamani kubadilishana korosho na kilo ya unga.
Akitolea majibu ya malalamiko hayo, Dkt. Kawambwa alibainisha ,kuhusu suala la uuzwaji wa korosho hawezi kulitolea taarifa kwani ni agizo kutoka serikali kuu linalowataka wakulima kupeleka katika maghala ili zinunuliwe na serikali na kudai atafuatilia suala hilo.