Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa,Abel Nyamahanga akiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga wakati wa ziara ya kamati siasa ya chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa ya kukagua miradi ya kimaendeleo mkoani hapo
mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga akinawa mikono kwenye moja ya maabara ya shule ya sekondari ya Mlamke iliyopo manispaa ya Iringa.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
KAMATI siasa ya chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa
kimeipongeza miradi inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa
kuwa na ubora unaotakiwa kutokana na dhamani ya pesa ambayo imetumika katika
miradi hiyo.
Akizungumza wakati wa kukagua miradi ya maendeleo katika
Manispaa hiyo Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa,Abel
Nyamahanga alisema kuwa kamati imefanikiwa kutembelea mradi wa uwanja wa
ndege wa nduli,bweni la shule ya sekondari ya Nduli,barabara ya Gangilonga,Machinjio
ya Ngelewala na maabara ya shule ya sekondari ya Mlamke wamekuta miradi hiyo
imekelezwa kwa kiwango kinachotakiwa.
Alisema kuwa kwa kipindi hiki ambacho manispaa ya Iringa
inaongwa na madiwani wa chama cha mapinduzi imekuwa inatelekeza vilivyo miradi
ya kukuza maendeleo kwa wananchi kwa kuitekeleza vilivyo Ilani ya chama hicho
ya mwaka 2020 hadi 2025.
Nyamahanga alisema kuwa viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa wamefanya kazi kubwa kuhakikisha wanazitumia fedha za wananchi vizuri
kwa kutekeleza ahadi za kutengeneza miradi kwenye ubora wake kulingana na
dhamani ya fedha ambayo imetolewa kwenye mradi husika.
Aidha Nyamahanga alisema kuwa licha ya kuridhishwa na miradi
mingi waliyoitembelea lakini wamekutana na miradi ambayo hawajaridhishwa nayo
kutokana na kutekelezwa chini ya kiwango na mingine kuwa na mapungufu mengi
ambayo wanatakiwa kulekebishwa haraka iwezekanavyo.
Alisema kamati haijaridhiwa na ujenzi wa maabara ya shule ya
sekondari ya Kleruu kwa kujengwa chini ya kiwango ukilinganishwa na thamani ya
fedha ambayo imetumika kwenye maabara hiyo ukilinganisha maabara nyingine
zilizojengwa kwenye shule nyingine.
Alisema kuwa katika mradi wa stand kuu ya mkoa wa Iringa
kunachangamoto ambayo wananchi walitoa ardhi katika eneo la mradi bado
hawajalipwa fidia zao ambazo wanadai hadi sasa wakati ofisi ya halmashauri ya
Iringa ikiwa inazo pesa za kuwalipa wananchi hao.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na ujenzi wa
uwanja wa ndege wa Nduli, Ujenzi wa bweni la wanafunzi shule ya sekondari
Nduli, Ujenzi wa Maabara shule ya sekondari Mlamke na Kleruu, Ujenzi wa
barabara ya lami ya Kihesa, Kikundi cha vijana mafundi selemala ‘YOUNG
FURNITURE GROUP’ cha Mlandege, Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Kigungawe,
Ujenzi wa jengo la abiria na utawala katika stendi mpya ya Igumbilo pamoja na
Mradi wa Machinjio ya kisasa wa Ngelewala
Kwa upande wake
mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga alisema kuwa wameyapokea maagizo yote
yaliyotolewa na kamati ya siasa ya chama chama mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa
na watayafanyia kazi ili kuondoa kasoro ambazo zimejitokeza kwenye baadhi ya
miradi ambayo kamati hiyo wameitembelea.
Aliwataka watendaji wote wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa weledi unaotakiwa ili kutumia fedha za
wananchi vizuri kuendana na mradi ambao unakuwa unatekelezwa kwenye maeneo yao.
Naye Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada
alisema kuwa kamati ya ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari ya Kleruu na
fundi aliyepewa kazi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanaijenga upya maabara hiyo
kwa kutumia fedha zao kwa sababu ya kujenga maabara hiyo chini ya kiwango huku
serikali ikiwa imetoa fedha zote zinazohitajika.
Alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanatekeleza miradi yote
kwa ubora na kubuni miradi mipya ambayo itasaidia kuchochea maendeleo ya
wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Ndg. Omary
Mkangama amesema moja ya sababu iliyopelekea kutokamilishwa kwa malipo ya fidia
kwa wananchi waliojitolea maeneo ni kufungwa kwa mfumo wa malipo tarehe
30.06.2021 nchi nzima kwaajili ya zoezi la usuluhishi wa kibenki na maandalizi
yakuingia kwenye mfumo mpya wa malipo MUSE ambapo zoezi hilo litakapokamilika
ndio Halmashauri itaanza kulipa na wananchi watalipwa baada ya mfumo wa malipo
kufunguliwa