Waziri Wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kilia) akifafanua jambo kwa baadhi ya waandishi wa habari toka mikoa mbalimbali nchini(hawapo pichani) wakati alipokuwa akifungua semina ya siku moja juu ya maadili na haki za binadamu mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa semina ya siku moja juu ya maadili na haki za binadamu, Tom Chilala akitoa neno la utangulizi kwa Waziri Wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (wa pili kushoto) wakati waziri huyo alipokuwa akifungua semina hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mtoa mada toka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Felister Mauya akitoa mada ya haki za binadamu kwa baadhi ya waandishi wa habari toka mikoa mbalimbali nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Anna Henga (kushoto) akifafanua jambo kwa baadhi ya waandishi wa habari toka mikoa mbalimbali nchini wakati semina ya siku moja juu ya maadili na haki za binadamu mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mgeni Rasmi, Waziri Wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mac D Promotion, Deogratius Rweyunga.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mac D Promotion, Deogratius Rweyunga akisisitiza jambo kwa baadhi ya waandishi wa habari toka mikoa mbalimbali nchini walioshiriki semina ya siku moja juu ya maadili na haki za binadamu mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari toka mikoa mbalimbali nchini wakimsikiliza Mgeni Rasmi, Waziri Wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani)wakati waziri huyo alipokuwa akifungua semina ya siku moja juu ya maadili na haki za binadamu kwa waandishi wa habari hao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Picha na WHUSM –Dar es Salaam.
************
Na. WHUSM –Dar es Salaam
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe
amewataka waandishi wa habari kote nchini kutokuwa dhaifu na wanyonge kwa
kutumiwa na mataifa ya nje kwa kupeleka taarifa za udhaifu na badala yake kuweka maslahi ya Taifa mbele.
Dk. Mwakyembe ameyasema hayo leo jijini Dar es Salam wakati alipokuwa akifungua semina ya siku moja kwa waandishi wa habari wa hapa nchini kuhusu maadili na haki za binadamu iliyoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa kushirikiana na taasisi ya Mac D Promotion.
“Kazi mnayoifanya ni kubwa sana na mmejenga majina makubwa sana, ni vema
mkalinda heshima zenu na kujenga madaraja na Serikali na sio nchi za nje kwani huo ni ulaji tu wa muda,” alisema Waziri Mwakyembe.
Dk. Mwakyembe amewataka waandishi kuandika habari za maendeleo yanayonekana katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya tano ikiwemo miradi mbalimbali iliyotekelzwa na ile inayotekelezwa.
Aidha Waziri mwakyembe aliongeza kuwa sheria iliyotungwa na serikali inawajali
waandishi wa habari na kuwahakikishia sheria hii itaboresha maslahi ya waandishi wa habari nchini.
Kwa upande wake Mwezeshaji katika semina hiyo ambaye pia ni mwandishi mkongwe, Allan Lawa, amewataka waandishi wa habari nchini kujiendeleza kitaaluma kwani mwandishi wa habari ni Yule aliyesoma.
“Sheria italeta maslahi sana, waandishi tusome, tusome sana, kwani mwandishi ni
yule aliyesoma,” alisema Lawa.
Semina hiyo ya siku moja yenye lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu
ya masuala maadili katika uandishi wa habari pamoja na kutambua haki za binadamu
pindi wanapoandika habari.