Home Mchanganyiko WAZIRI HASUNGA ATEMBELEA “KIJIJI CHA USHIRIKA” KWENYE MAONESHO YA NANENANE, 2019

WAZIRI HASUNGA ATEMBELEA “KIJIJI CHA USHIRIKA” KWENYE MAONESHO YA NANENANE, 2019

0

*************************

Waziri wa Kilimo Mhe.Japhet Hasunga ametembelea mabanda ya wanaushirika
kwenye “Kijiji cha Ushirika” katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa
Mkoani Simiyu ambayo yamefunguliwa rasmi na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Maonyesho hayo yenye kauli mbiu “Kilimo, Mifugo na Uvuvi katika Ukuaji wa Uchumi wa Nchi”.

Katika Maonesho hayo, Vyama vya Ushirika wa aina mbalimbali Ushirika wa Mazao
(Pamba, Tumbaku, Kahawa) Ushirika wa Umwagiliaji, SACCOS, Ushirika wa Maziwa, Ushirika wa Wafugaji Nyuki na Ushirika wa Wavuvi.

Pamoja na mambo mengine, Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa kushirikiana na
wadau, taasisi zinazoshughulika na masuala ya ushirika inaendesha mafunzo ya
Ushirika katika “Kijiji cha Ushirika” ambapo Wanachama, Viongozi na Watendaji wa Vyama vya Ushirika wanapa fursa ya kujifunza masuala muhimu ya Ushirika