Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu akiwa ameambatana na Viongozi wa Mkoa na Wilaya wakati akikagua ujenzi wa madarasa ya Shule ya Sekondari ya Ugala River, iliyopo katika Kata ya Ugala, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Mkoani Katavi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja viongozi wa Mkoa na Wilaya kwenye nyumba ambayo wanaishi waalimu wa shule ya sekondari Ugala River, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Kigoma.
Madarasa yanayojengwa katika shule ya Sekondari ya Ugala River katika Kata ya Ugala, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi lengo ni kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule hiyo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu akiwa ameambatana na Viongozi wa Mkoa na Wilaya wakati akikagua ujenzi wa maabara ya Shule ya Sekondari ya Ugala River, iliyopo katika Kata ya Ugala, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Mkoani Katavi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu akiongea na waalimu pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Ugala (hawapo pichani) wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa madarasa pamoja na maabara ya Shule ya Sekondari ya Ugala River, iliyopo katika Kata ya Ugala, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Mkoani Katavi
………………………………………………………………………
Na. Angela Msimbira NSIMBO- KATAVI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu alisema Serikali imejiwekea mkakati katika Sekta ya Elimu kwa kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi kwa waalimu wanaofanyakazi katika maeneo magumu na mbali kufikika
Aliyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na maabara katika shule ya Sekondari ya Ugala River iliyopo katika kata ya Ugala, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi
Waziri Ummy alisema katika kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ya kujifunza na kufundishia Serikali imejikita katika kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ya waalimu wanaotoka mbali kupata maeneo ya kuishi.
“ Wapo waalimu ambao wanatoka mbali mfano mzuri ni hapa shule ya Sekondari Ugala River yupo mwalimu ametokea Kilimanjaro na kaamua kuja kufanyakazi katika Kata ya Ugala, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi, Ni wajibu wa Serikali na wananchi wa maeneo husika kuhakikisha wanaboresha mazingira ili waweze kubaki muda mrefu katika maeneo wanayofanyia kazi.” Alisema Mhe Ummy
Alisema Serikali inawatia moyo waalimu wote ambao wanafanyakazi katika maeneo magumu hasa katika kata za mbali na kuahidi kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samiah Hassan Suluhu itawekeza katika kuboresha mazingira ya watumishi nchini
Kuhusu Nyumba za waalimu katika Shule ya Sekondari Ugala RWaziri Ummy alisema katika kuunga mkono juhudi za wananchi Serikali itatoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya watumishi ambayo itachukua familia nne kwa pamoja. Lengo ni kuwatia moyo waalimu wanaofanyakazi katika maeneo ya mbali
Kuhusu ajira za waalimu wapya alisema Selikali ilitoa kipaombele kwa Halmashauri zenye maeneo yenye changamoto na maeneo ya mbali kufikika , jambo hili limetekelezwa kwa asilimia 100 ambapo kwa shule ya Sekondari ya Ugala River imepata waalimu wa Sayansi 3.
Aidha, amesema Serikali ya awamu ya sita imeamua kujikita katika kuimarisha maeneo magumu kama Halmashauri ya Nsimbo ambapo waalimu wapya wa Sayansi 26 wamepangwa katika Halmashauri hiyo