Home Mchanganyiko SERIKALI YASHAURIWA KUWEKA NGUVU KWENYE KUWEZESHA VIFAA VYA MASOMO YA SAYANSI

SERIKALI YASHAURIWA KUWEKA NGUVU KWENYE KUWEZESHA VIFAA VYA MASOMO YA SAYANSI

0

Mwalimu
wa Taaluma wa Shule ya Sekondari Coastal High School, Isaack Dastan
Kifwete wakati mkutano wao baina yao na waandishi wa habari uliokuwa na
lengo la kueleza  siri iliyowafanya kung’ara kwenye matokeo ya kidato
cha sita 2020/2021 kushoto ni Mwalimu wa Taaluma Msaidizi wa Shule ya Sekondari Coastal High Shool Moses Mhina
Mwalimu
wa Taaluma Msaidizi wa Shule ya Sekondari Coastal High Shool Moses
Mhina akizungumza wakati wa mkutano huo kushoto ni Mwalimu
wa Taaluma wa Shule ya Sekondari Coastal High School, Isaack Dastan
Kifwete

Mwalimu
wa Michezo na Klabu za Jamii kwenye shule  hiyo akieleza namna michezo
inavyochangia ufaulu kwa wanafunzi Salim Mwakumuna kushoto ni Mwalimu
wa Taaluma wa Shule ya Sekondari Coastal High School, Isaack Dastan
Kifwete

Sehemu ya walimu wa shule ya Sekondari Coastal High School wakiendelea na majukumu yao kama walivyokutwa

Mwalimu
wa Taaluma wa Shule ya Sekondari Coastal High School, Isaack Dastan
Kifwete akikagua madaftari ya wanafunzi kama inavyoonekana

 

SERIKALI imeshauri kuweka juhudi kubwa kuwezesha vifaa vya kufundishia
ambavyo vitasaidia kuwa na wanasayansi halisi kwa kusoma kwa vitendo ili
kuweza kuendana na uchumi wa viwanda.

Iwapo vifaa vya masomo ya
sayansi vitakuwepo kwenye shule mbalimbali hapa nchini itawawezesha
wanafunzi kuweza kusoma kwa vitendo na hivyo kuongeza ufaulu na hatimaye
kuwa na wataalamu wengi

Hayo yalisema na Mwalimu
wa Taaluma wa Shule ya Sekondari Coastal High School, Isaack Dastan
Kifwete wakati mkutano wao baina yao na waandishi wa habari uliokuwa na
lengo la kueleza  siri iliyowafanya kung’ara kwenye matokeo ya kidato
cha sita 2020/2021..

Shule hiyo imefanya vizuri katika matokeo
hayo  baada ya Wanafunzi kuwa na ufaulu wa Daraja la Kwanza na Pili tu
(Division I na II)yaliyopatikana shuleni hapo na kuifanya kuwa ya kwanza
katika wilaya ya Tanga.

Alisema matokeo hayo yamewawezesha
kuendelea kuwa shule ya kwanza(Namba 1)katika wilaya ya Tanga mjini huku
wakiwa shule ya nne(Namba 4) kwa mkoa wa Tanga.

Aidha alisema
mafanikio hayo yamechagiwa na uongozi pamoja na walimu walio bora
ikiwemo kujituma bila kuchoka na wanafunzi kuwa na ari katika masomo.

“Kwanza
ni ushirikiano kutoka kwa Mkurugenzi wa Shule hii Mathew Marupa kuwa na
walimu bora na wanajitoa kwa muda wote hali hii imesaidia kuwezesha
kupata matokeo mazuri”Alisema

Alisema pia ni kuwekwa kwa bidii
kwenye masomo wanayosimamia pamoja na kuwa na wanafunzi wanaojitambua
ambapo pale wanapofika wanapewa malengo ya shule kuwa hautakiwi kufeli
unapokua kwenye shule hii”alisema Kifwete.

Aidha alisema kwa
miaka minne mfululizo shule hiyo imeendelea kufanya vizuri kwa kuwa
wanafunzi wanakuwa katika mazingira bora ya kujifunza na hivyo kupelekea
kuelewa kila wanachofundishwa.

Awali akizungumza katika mkutano
huo,Mwalimu Msaidizi wa Taaluma Moses Mhina ambaye pia ni Mkuu wa Idara
ya Sayansi anafundishi masomo ya Kemia na Biologi alisema matokeo ya
kidato cha sita wanakuwa wakifanikiwa kutokana na uwepo wa nidhamu ya
hali ya juu ambalo kwao ndio jambo la kwanza kabla ya taaluma.

Alisema
wanafunzi wanapofika shuleni jambo la kwanza ni nidhamu,la pili ni
ushirikiana kati ya walimu na wafanyakazi wengine,kujitoa ni jambo
ambalo ni kubwa sana kwao na wakati mwengine kufanya kazi nje ya muda wa
kazi na kuwafundisha wanafunzi kwa waledi ambao unawatengenezea
ujasiri.

“Lakini pia ushirikiano walimu na watu wa nje ambao sio
walimu hasa wazazi na walezi kwa sababu kunaweza kutokea changamoto ya
utoro lakini tunapokutana na wazazi na kuwaeleza utoro unavyokwamisha
matokeo mazuri na hivyo wao kutupa ushirikiano “Alisema

Alisema
siri nyengine ambayo imewasaidia wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi
kufanya vizuri ni kuwatengenezea mtazamo chanja unajua kwenye malezi
wanayolelewa mtu tangia akiwa mdogo anasikia habari kwa kaka zake kwamba
sayansi ni ngumu lakini wao wanafunzi wanapofika shuleni wanawaelezwaa
namna wanavyuoweza kufanya masomo hayo bila woga na hivyo kuwafundisha
wanafunzi kwa vitendo .

Mwalimu huyo alieleza kwamba hatua
inayoondolea woga kwao na hivyo kuwajengea namna ya kujiamini na
kumtengeneza ujasiri wa kujibu maswali na hivyo kuwawezesha kufanya
vizuri wanapokuwa kwenye mitihani yao.

“Lakini pia tumekuwa
tukifanya ziara ya kutembelea kwenye viwanda na hivyo kuona namna
sayansi inayoweza kufanya kazi na hivyo kuwawezesha wanafunzi kupata
uelewa mpana “Alisema

Hata hivyo pia siri nyengine ni wao
kujitahidi kufundisha kwa waledi na kutoa mazoezi ya kutosha kwa
wanafunzi yanayowapa ujasiri wa kutambua mambo mengi na hivyo
kuwawezesha kutimiza ndoto zao za kufanya vizuri.