AFISA Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando na Mwenyekiti wa Yanga SC, Dkt. Mshindo Msolla, wakisaini mkataba wa mashirikiano ya maudhui wenye thamani ya Shilingi bilioni 41 pamoja na VAT kwa kipindi cha miaka 10.
Klabu ya Yanga imeingia mkataba wa maudhui na Azam Media wenye thamani ya Sh41 bilioni pamoja na kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa kipindi cha miaka 10.
Mkataba huo umesainiwa leo Alhamisi Julai 8, 2021 jijini Dar es Salaam na mkurugenzi mtendaji wa Azam Media, Tido Mhando na mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla.
Kwa mujibu wa mkataba huo, Yanga itapokea Sh200 milioni kwa mwezi kwa msimu ujao, fedha ambayo itakuwa ikiongezeka kila msimu.
Pia, Azam Media itatoa bonasi ya Sh44.4 bilioni kwa miaka 10, endapo klabu hiyo itamaliza ligi ikiwa katika nafasi ya kwanza au ya pili katika kila msimu.