Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko TEMDO, Dkt. Sigisbert Mathias Mmasi akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) Dkt. Sigisbert Mathias Mmasi akizungumza na wananchi waliotembelea Banda la TEMDO katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) Dkt. Sigisbert Mathias Mmasi (kushoto) akiwaelezea jinsi mashine inavyofanya kazi wananchi waliotembelea Banda la TEMDO katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
……………………………………………………….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) imejipanga kuanza kubuni na kuzalisha vifaa vya hospitali ikiwemo vitanda vya aina yote ambavyo vitaondoa uhaba wa ukosefu wa vitendea kazi katika hospitali mbalimbali hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko TEMDO, Dkt. Sigisbert Mathias Mmasi amesema kuwa kuanzia mwaka 2022 wataaza kuuza vifaa vya hospitali vya kisasa kwa ajili ya kutoa huduma kwa Jamii.
“Wizara ya Afya tayari wametupa barua kwa ajili ya kuanza kuzalisha vifaa vya hospitali ambavyo vitakuwa sehemu ya kutatua changamoto ya vitendea kazi katika hospitali” amesema Dkt. Mmasi.
Dkt. Mmasi amesema kuwa TEMDO pia wanamashine za aina mbalimbali za kisasa za viwandani ikiwemo mashine za kusanga karanga, matunda, unga wa lishe pamoja na viungo vya kupikia.
“Tumetengeneza mashine zaidi ya 40 za kisasa ambazo zinauwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa katika viwanda” amesema Dkt. Mmasi.
Amesema kuwa taasisi ya TEMDO ina uwezo wa kufunga mitambo katika viwanda vikubwa kwa ufanisi ikiwemo viwanda vya kutengeneza pamba na bia.
Dkt. Mmasi ameeleza kuwa TEMDO ina wahandisi wenye uwezo mkubwa katika fani tofauti kwa ajili ya kuchora ramani ya kufunga mitambo ya kisasa katika viwanda kwa gharama nafuu.
“TEMDO tunatoa mafunzo ya namna kuendesha mitambo ya kisasa katika viwanda kupitia mashine kwa ajili ya kuzalisha bidhaa mbalimbali ambazo wanatumia” amesema Dkt. Mmasi.
TEMDO ni Taasisi ya Uhandisi na Ubunifu Mitambo Tanzania iliyopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo ilianzisha na serikali mwaka 1982 kwa lengo la kubuni na kusanifu mitambo.
Baada ya kuanzishwa taasisi TEMDO imeruhusiwa kunakiri teknolojia kutoka nje ya nchi bila kushitakiwa kwa lengo la kuendana na teknolojia ya sasa kulingana na uwitaji wa wa Taifa.