Home Michezo KANE AING’ARISHA ENGLAND YAICHAPA 2-1 DENMARK NA KUTINGA FAINALI EURO 2020

KANE AING’ARISHA ENGLAND YAICHAPA 2-1 DENMARK NA KUTINGA FAINALI EURO 2020

0

ENGLAND imetinga fainali ya Euro 2020 baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Denmark katika mchezo uliodumu kwa dakika 120 Uwanja wa Wembley Jijini London.
Pamoja na Denmark kutangulia kwa bao la kiungo wa Sampdoria, Mikkel Damsgaard dakika ya 30, lakini beki wa AC Milan, Simon Kjær akajifunga dakika ya 39 akijaribu kuokoa mpira wa mshambuliaji wa Manchester City, Raheem Stering kuipatia England bao la kusawazisha.
Zikaongezwa dakika 30 baada ya kutimia dakika 90 na ndipo mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akaifungia bao la ushindi England dakika ya 104 akimalizia mpira uliookolewa na kipa wa Leicester City, Kasper Peter Schmeichel baada ya yeye mwenyewe kupiga penalti kufuatia Sterling kuangushwa kwenye boksi.

Inakuwa mara ya kwanza Three Lions kuingia fainali ya michuano mikubwa tangu walipofika fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1966 na watakutana na Italia Jumapili hapo hapo Wembley.
Ikumbukwe Italia iliitoa Hispania usiku wa kuamkia leo hapo hapo Wembley kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 120.