Timu ya Tanzania (Taifa Stars) imeng’ara katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kwa kuichapa Timu ya taifa ya Malawi, ‘The Flames’, mabao 2-0 Mchezo wa kirafiki.
Baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza, Taifa Stars ilipata Mabao kupitia kwa Mshambuliaji hatari John Bocco dakika ya 68 akipokea pasi kutoka kwa Denis Kibu na Benki Patrick Israel Mwenda dakika ya 75 Mpira wa Faulo baada ya Denis Kibu kichezewa rafu.