Home Mchanganyiko WAJUMBE KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YATEMBELEA KIWANDA...

WAJUMBE KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YATEMBELEA KIWANDA CHA SIGARA TANZANIA (TCC) NA KIWANDA CHA KNAUF KINACHOZALISHA GYPSUM BOARD

0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akifafanua jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati kamati hiyo ilipotembelea Kiwanda cha Sigara (TCC) kwa ajili ya kuona utekelezaji wa masuala ya Usalama na Afya katika maeneo mbalimbali ya kazi. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Najma Giga Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga.

Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakisikiliza maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) walipotembelea Kiwanda cha Sigara (TCC) kwa ajili ya kuona utekelezaji wa masuala ya Usalama na Afya katika maeneo mbalimbali ya kazi, Jijini Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Najma Giga akizungumza wakati kamati hiyo ilipotembelea Kiwanda cha Knauf kinachozalisha Gypsum, Mkuranga Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Sheria kutoka Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) Bw. Godson Killiza akieleza jambo Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipotembelea kampuni hiyo kwa ajili ya kuona utekelezaji wa masuala ya Usalama na Afya katika maeneo mbalimbali ya kazi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Najma Giga (wa pili kutoka kushoto), Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (kulia) na Mkurugenzi wa Uhusiano TCC, Bi. Patricia Mhando wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na Wataalamu kutoka Kampuni ya TCC.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipofanya ziara katika Kampuni ya Sigara (TCC) kwa ajili ya kuona utekelezaji wa masuala ya Usalama na Afya katika maeneo mbalimbali ya kazi.

Mkurugenzi wa Uhusiano Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC), Bi. Patricia Mhando (wa tatu kutoka kushoto) akimuonesha Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Najma Giga bidhaa zinazozalishwa na Kampuni hiyo. Wa tatu kutoka kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa ameongozana na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria mara baada ya kuwasili katika Kiwanda cha Knauf kinachozalisha Gypsum, Mkuranga Jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Kiwanda cha Knauf Bw. Armen Muradov (wa pili kutoka kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa ajili ya kuona utekelezaji wa masuala ya Usalama na Afya katika maeneo mbalimbali ya kazi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, wafanyakazi kutoka OSHA na Kiwanda hicho cha Knauf kinachozalisha Gypsum, Mkuranga Jijini Dar es Salaam.

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(SERA, BUNGE, URATIBU, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)