………………………………………………………………..
Mashindano ya riadha ya mbio za mita 100 fainali maalum zimefanyika leo katika uwanja wa chuo cha ualimu Mtwara.
Washindi malimbali wamepatikana katika mbio hizo na kujizolea medali.
Sambamba na hilo, pia mbio za mita 100, wavulana na wasichana hatua makundi, kurusha tufe kwa wavulana na wasichana, mbio za mita 200, mita 1500 na mbio za kupokezana kijiti 4 x mita 100 kwa wavulana na wasichana z.
Mikoa ya Mwanza, Geita, Shinyanga na Mara ilitia fora katika hatua hii kufuatia wanariadha wake wengi kufanya vizuri katika hatua ya mchujo na hivyo kufanikiwa kusonga mbele.
Mashindano ya riadha yaliyoanza leo yataendelea kufanyika hadi tarehe 18/6/2021 ambapo washindi mbalimbali watajinyakulia medali na vikombe.