Home Mchanganyiko KATIBU MKUU MAJI AISISITIZA MATUMIZI YA MFUMO  JUMUISHI WA KUSIMAMIA ANKARA ZA...

KATIBU MKUU MAJI AISISITIZA MATUMIZI YA MFUMO  JUMUISHI WA KUSIMAMIA ANKARA ZA MAJI

0
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akikufunga mafunzo yaliyolenga kutoa uelewa wa pamoja juu ya kusimamia huduma za ankara za wateja wa Maji yaliyofanyika mjini  Tabora .
………………………………………………………………………..

NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

KATIBU Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga amewataka wataalamu wa Teknolojia ya habari na Mawasiliano(TEHAMA) kuhakikakisha Mfumo  Jumuishi wa Kusimamia Ankara za Maji kwa Mamlaka za Maji nchini uwe unapatikana masaa 24 kwa siku zote.

Alisema mfumo mpya wa pamoja wa utoaji Ankara za Maji umeonesha manufaa kwa Mamlaka ambazo zimeanza kuutumia kutokana na kuondoa changamoto nyingi ikiwemo gharama na usalama wa taarifa za wateja.

Mhandisi Sanga alitoa kauli hiyo ana wakati wa kufunga mafunzo yaliyolenga kutoa uelewa wa pamoja juu ya kusimamia huduma za ankara za wateja wa Maji yaliyofanyika mjini  Tabora .

Alisema mfumo huu ni wa uhakika na salama kwa kuwa  umetengenezwa na wataalamu wa ndani Mamlaka ya Serikali Mtandao na unakidhi mahitaji ya serikali kwa sasa.

“Mifumo mingine iliyopo kwenye Mamlaka za Maji nchini sehemu kubwa inamilikiwa na watu wa nje na ilikuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wateja …hii ni hatari na tena inagharama na wakati mwingine ukichelewa kuhuisha leseni yako anaweza ku block uziweze kufanya kazi zao”alisema

Alisema kufuataia hali hiyo Wizara na Sekta ya Maji  kwa kushirikiana  na e GA wameamua kutengeneza Mfumo  Jumuishi wa Kusimamia Ankara za Maji ili kuepukana na changamoto mbalimbali zinazoweza kusababu huduma isiyobora kwa wananchi.

Mhandisi Sanga alisema lazima kuweo na mpango wa kunusuru mfumo huo pindi kunapotokea majnga ili kutoathiri makusanyo ya fedha na kuwasababishia wananchi kukosa huduma na kuleta kero.

Awali Mratibu wa mafunzo Mhandisi Masoud Almas alisema mafunzo hayo yalilenga kuhakikisha Mamlaka zote nchini zinaanza kutumia Mfumo  Jumuishi wa Kusimamia Ankara za Maji na kuondokana na mifumo ya wakandarasi binafsi.

Alisema hadi hivi sasa Mfumo huo unatumiwa na Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira 46 kati ya 95 ikiwa ni sawa na asilimia 48.

Alisema lengo ni kuhakikisha Mamlaka zote zinapewa mafunzo ya kutumia mfumo ili hatimaye utumike nchi nzima.

Alizita faida za mfumo huo kwamba taarifa zote za mteja zinaweza kupatikana kwa nia ya mtandao  , kupitia kompyuta au simu yake ya mkononi na mteja anaweza kununua maji kupitia Simu ya mkononi.