CHAMA Cha Mapinduzi(CCM),Mkoa wa Dar es Salaam, kemewaita Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Siporah Liana na Meya wa Manispaa hiyo Songoro Mnyonge kufuatia kutupiana maneno wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani, hivi karibuni.
Katibu wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shaibu Akwilombe, amesema Kamati ya Siasa ya Chama, Mkoa, itawata kesho na kuwahoji Meya na Mkurugenzi ambapo pia Mkuu wa Mkoa huo Amos Makala aitashiriki.
“CCM hairidhishwi na uhusiano baina ya awatendaji wa halmashauri na Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kinoni,”alisema Akwilombe.
Ameyasema hayo wakati wa kuhitimisha ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, kukagua miradi ya maendeleo ya Chama na ya Serikali katika Wilaya ya Kinondoni.
Akwilombe alisema, licha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Amos Makala kujaribu kuingilia kati sakata hilo lakini Chama kitaita pande zote ambazo ni baraza la madiwani na halmashauri ya manispaa, ili kujua kiini cha uhusiano huo mbovu na kutoa maelekezo .
Alisema katika suala hilo CCM itachukua hatua stahiki kwa wahusika.
” Uhusiano huo mbovu uliopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, umeanza kuathiri maendeleo ya halmashauri hiyo jambo ambslo linakwamisha utekelezaji wa Ilani ya Chama,”alibainisha Akwilombe.
“Tumeambiwa hivi sasa kuna ukaguzi maalumu wa hesabu unaendelea katika halmashauri.Hii ikifanyika inathibitisha kuwa katika manispaa ya Kinondoni hawaaminiani na miradi itasimama tu ili kupisha ukaguzi huo.Hatuewezi kwenda hivyo”alisema Katibu huyo wa Chama,”Katibu huyo wa Chama.
Akwilombe alibaendelea kusema, mgogoro huo unaathiri utekelezaji wa Ilani ya CCM hivyo hawatasita kuchukua hatua stahiki ili halmashauri hiyo iwatumikie wananchi kwa maslahi ya Taifa.
“Katika uongozi hakuna jambo baya kama kuona wote walio kutangulia walikuwa hawafai.Ieleweke kuwa sisi wote ni binadamu na kila binadamu anamapungufu yake,”alieleza Katibu huyo.
Mjumbe wa Hakmshauri Kuu ya CCM (NEC) Yusuf Nasoro,alisema mgogoro huo wa kiutendaji katika Manispaa hiyo haukubariki na Chama kitachukua hatua.
“Kamati ya Siasa ya Mkoa imewaita na tutawahoji ili kujua nini kinaendelea katika halmashauri hii.Chama hakijafurahishwa na hali hii”alisema Nasoro.
Hivi karibuni wakati wa kikao cha baraza la madiwani katika halmashauri hiyo yaliibuka majibizano makali baina ya Mkurugenzi Sipora na Meya Mnyonge ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Makala alilazimika Kuwaita na kujaribu kiwasuluhisha.