Kutoka kushoto ni katibu tawala wa mkoa wa Iringa Happiness Seneda katika ni mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William wakiwa kwenye kikao na wakuu wa taasisi za UMMA za mkoani Iringa.
katibu tawala wa mkoa wa Iringa Happiness Seneda,mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga na Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa taasisi za UMMA za mkoani Iringa.
katibu tawala wa mkoa wa Iringa Happiness Seneda,mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga na Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa taasisi za UMMA za mkoani Iringa.
katibu tawala wa mkoa wa Iringa Happiness Seneda,mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga na Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa taasisi za UMMA za mkoani Iringa.
Na Fredy Mgunda,Iringa
WATUMISHI wa UMMA mkoa Iringa
wametakiwa kuwa mfano kwa wananchi kwa kuhakikisha wanakuwa na mashamba ya
kimkakati yatakayowasaidia wananchi kujifunza ikiwa ni pamoja na wao kujiinua
kiuchumi .
Akizungumza kwenye kikao cha wakuu
wa taasisi za UMMA za mkoa wa Iringa cha kujitambulisha kwa mkuu wa mkoa mpya
Queen Sendiga,katibu tawala wa mkoa huo Happiness Seneda alisema kuwa mkoa wa
Iringa umebarikiwa kuwa na ardhi ambayo inafaa kwa kilimo cha mazao yoyote yale
Seneda alisema kuwa watumishi
wengi wa umma wamekuwa na hali ngumu kutokana na kutowekeza kipato chao katika
ardhi jambo linalowaletea ugumu hasa pale wanapopata matatizo ya kufiwa au
kufariki wao wenyewe.
Aliongeza kusema kuwa watumishi
wengi wa Umma wamekuwa wakijikita katika vitendo vya anasa kama ulevi na uzinzi
hali inayosababisha mishahara yao kutumika bila malengo na kuzifanya familia
zao kuishi katika mazingira magumu.
“Watumishi wenzangu wa sekta za
umma tunajisahau kwa sababu tunakuwa na uhakika wa kupata mishahara na malupulupu
basi tumekuwa ni wanywaji pombe wa kupindukia tumekuwa wazinifu mwisho wasiku
tunapata tabu pale mnapofariki maana unakuta nyumbani hakuna hata kitu cha
kuanzia” alisema Seneda
Awali akizungumza mkuu wa mkoa wa
Iringa Mh. Queen Sendiga alisema mkoa umejipanga kuja na kilimo mkakati
kitakachowainua wananchi kiuchumi hivyo watumishi wa umma wanatakiwa kuwa mfano
kwa kuwa na mashamba ya kilimo cha biashara.
Alisema ni aibu kwa mkoa wa
Iringa kuonekana wananchi wake wanalia umasikini wakati mkoa umebarikiwa kuwa
na ardhi yenye rutuba inayozalisha mazao ya aina mbalimbali kama alizeti,
nyanya, palachichi, mpunga mahindi na mengineyo.
Sendiga alisema mkakati walionao
ni kuona kila kaya inakuwa na mashamba ya kulima na katika mashamba hayo eka
moja ni lazima liwe shamba la kilimo maalumu cha biashara ili kuwainua wananchi
wake.
‘’Niseme wazi ninachukizwa na
hali ya wananchi wa mkoa wa Iringa wakati wamerikiwa ardhi yenye rutuba nyingi
ya kilimo mkoa sasa umekuja na mkakati wa kuhakikisha kila kaya inakuwa nae ka moja
ya kilimo maalumu cha zao la biashara na nitafuatilia hilo ukiona umelima kilimo
kile cha mazoea hakikisha una eka moja ya kilimo biashara”alisema Sendiga.
Wakizungumza baadhi ya wakazi wa
mkoa wa Iringa wamesema kuwa mkakati aliokuja nao mkuu wa mkoa ni mzuri na
utawainua wananchi wa mkoa wa Iringa ambao wamekuwa wakilima kilimo cha mazoea japo changamoto huwa katika suala la pembejeo.