Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso akisikiliza kero za wananchi wa kijiji cha Berege kilichopo Wilaya ya Mpwapwa waliosimamisha msafara wake wakati ziara yake ya kukagua utekelezaji na uendeshaji wa miradi ya maji wilayani humo.
Meneja wa RUWASA Mpwapwa, Mhandisi Syprian Warioba,akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maji iliyopo wilayani humo kwa Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (hayupo pichani) wakati ziara yake ya kukagua utekelezaji na uendeshaji wa miradi ya maji wilayani humo.
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Berege kilichopo Wilaya ya Mpwapwa wakati ziara yake ya kukagua utekelezaji na uendeshaji wa miradi ya maji wilayani humo pamoja na kusikiliza kero zao.
Wananchi wa kijiji cha Berege wakimsikiliza Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso,wakati akizungumza nao na wakati ziara yake ya kukagua utekelezaji na uendeshaji wa miradi ya maji wilayani humo pamoja na kusikiliza kero zao.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabiri Shekimweri,akizungumza mara baada ya kupokea maagizo ya Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso,aliyoyatoa katika kijiji cha Berege wakati ziara yake ya kukagua utekelezaji na uendeshaji wa miradi ya maji wilayani humo pamoja na kusikiliza kero zao.
Mbunge wa jimbo la Mpwapwa (CCM) Mhe.George Malima akizungumza na wananchi wa kijiji cha Berege wakati wa ziara ya Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, ya kukagua utekelezaji na uendeshaji wa miradi ya maji wilayani humo pamoja na kusikiliza kero zao.
Baadhi ya wanakijiji wa Berege wakitoa kero zao kwa Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso,wa wakati ziara yake ya kukagua utekelezaji na uendeshaji wa miradi ya maji wilayani humo pamoja na kusikiliza kero zao.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Berege wakifatilia hotuba ya Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso,(hayupo pichani) wakati akizungumza nao alipofanya ziara yake ya kukagua utekelezaji na uendeshaji wa miradi ya maji wilayani humo pamoja na kusikiliza kero zao.
…………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso,ameagiza kuvunjwa kwa Jumuiya ya Maji katika kijiji cha Berege huku akitoa onyo kali la ubadhilifu wa fedha za Jumuiya ya watumia maji katika mradi wa maji kijijini hapo.
Kauli hiyo ametoa Mhe.Aweso wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji na uendeshaji wa miradi ya maji pamoja na kuzungumza na wananchi katika kijiji cha Berege kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.
Waziri Aweso alipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na jumuiya ya watumiaji maji katika Kijiji cha Berege kuwa fedha zinakusanywa bila ya kupelekwa benki na hivyo kulazimika kuivunja jumuiya hiyo.
“Nimebaini fedha za Jumuiya ya Watumia Maji hapa Berege zinaliwa na hakuna usimamizi mzuri wala utunzaji mzuri wa taarifa za fedha, hivyo nakuagiza Mkuu wa Wilaya ufanyike ukaguzi maalum (special audit) katika akaunti ya Jumuiya hii ili kuweza kubaini fedha zote zilizoliwa na hatua kali zichukuliwe” amesema Aweso
Amesema kuwa lengo la kuwa na jumuiya hizo ni kuhakikisha fedha inayokusanywa inatunzwa ili kufanyia ukarabati pindi tatizo dogo linapojitokeza na kuongeza vituo vya kuchotea maji jambo ambalo limeshindwa kufanyika.
“Jumuiya hii naivunja mara moja haifai maana imeshajifia tayari,Mkuu wa wilaya vyombo vya usalama vipo,kama kuna fedha imeliwa basi wahusika wazitapike ili hili liwe funzo kwa Jumuiya nyingine zote nchini,”amesistiza.
Waziri Aweso amesema kuwa Jumuiya za Watumia Maji nchini zimekuwa zinaajiri watu wasiokuwa na sifa, hivyo amesisitiza kuwa kuanzia sasa Jumuiya zote za watumia maji nchini ziajiri mafundi sanifu wanaomaliza kutoka Chuo cha Maji na kuajiri Wahasibu wenye sifa ya Uhasibu.
“Jumuiya nyingi za maji zimekuwa zikivunjika kutokana na changamoto za watu kuingia na kujichukulia pamoja na kula pesa za uendeshaji wa miradi ya maji, niwahakikishie wananchi wote waliokula fedha za mradi huu na maeneo mengine nchini wajue watazitapika,” amesema Aweso
Aidha ametoa onyo kwa Jumuiya za Watumia Maji nchini kuacha tabia ya kuajiri watu wasiokuwa na sifa na badala yake waajiri wahasibu na Mafundi Sanifu wenye sifa na kuhakikisha taarifa za mapato na matumizi ya fedha zinatolewa kila wakati.
Pia amemuagiza Meneja wa RUWASA Mpwapwa, Mhandisi Syprian Warioba kurejesha fedha zilizochukuliwa katika Jumuiya ya Watumia Maji Berege kuwalipa wataalam kwa ajili ya usimamizi wa miradi kwa kuwa serikali imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya kazi hiyo.
Hata hivyo amemuagiza Meneja wa Wakala wa Uchimbaji Visima (DDCA) Peter Mdalangwila kuhakikisha wanafika Mpwapwa Jumamosi Mei 29, 2021 kuchimba visima vitatu katika Wilaya hiyo na kati ya visima hivyo kimoja kichimbwe katika Shule ya Sekondari Berege ili kupunguza adha ya maji inayowakabili wanafunzi shuleni hapo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Shekimweri amesema kuwa amepokea maelekezo na kuahidi kuunda kamati ili ifanyie uchunguzi mradi huo.