Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini mkoani Iringa Bw. Richard Kasesela akishuhudia mpambano mkali wa SAMAKIBA timu zinazoundwa na Mchezaji wa soka wa Kimataifa mtanzania Mbwana Samatta anayechezea timu ya Fenerbahce ya Uturuki na mwanamuziki maarufu nchini Tanzania na Ukanda wa Afrika kwa ujumbla Ali Kiba zilizochuana kwenye uwanja wa Samora mkoani humo akihudhuria na wasanii mbalimbali maarufu nchini.
Mpambano huo ambao timu hizo zilitoka sare ya 1-1 kwa upande wa timu ya Samatta goli lilifungwa na Badibanga kutoka Marekani rafiki wa Samatta na goli la upande wa Ali Kiba lilifungwa na mchezaji Thomas Tirshan.
Mchezo huo ulidhaminiwa na kiwanda kukibwa cha maziwa nchini cha ASAS DAIRIERS cha mkoani Iringa ambapo michuano hiyo inafanyika kila mwaka kwa lengo la kukusanya fedha na kusaidia jamii zenye mazingira magumu.
Vijana hao wenye uzalendo kwa nchi yao waliamua kuungana na kuunda timu zao pamoja na washirika wao ili kufanya tamasha la mchezo wa mpira wa miguu ili fedha inayopatikana irudishwe kwa jamii kwa lengo la kusaidia wananchi wenye mahitaji muhimu katika jamii, Na safari hii wamedhamiria kusaidia baadhi ya vituo vya watoto wenye mazingira magumu na yatima mkoani Iringa.
Vijana wa kikosi cha Ali Kiba na Mbwana Samatta wakiwa katika mstari kwa ajili ya kukaguliwa kabla ya kuanza kwa mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa Ijumaa.
Timu hizo zikichauana vikali kwenye uwanja wa Samora mkoani Irinda.
Baadhi ya mashabiki wakishuhudia chezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.
Mchezaji wa Tanzania wa Kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta anayechezea timu ya Fenerbahce ya Uturuki akiwasiliana na wachezaji wenzake wakati mchezo huo ukiendelea kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa ijumaa mwishoni mwa wiki hii.
Mwanamuziki Ali Kiba akinyanyuliwa na mchezaji wa timu ya Mbwana Samatta mara baada ya kuangkuka wakati mchezo huo ukiendelea.
Mchezaji wa Tanzania wa Kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta anayechezea timu ya Fenerbahce ya Uturuki akijiandaa kupiga mpira uliotengwa wakati mchezo huo ukiendelea kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa
Kikosi cha timu ya Ali Kiba kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Makapteni wa timu za Ali Kiba na Mbwana Samatta wakiwa katika picha ya pamoja na waamuzi wa mchezo huo kabla ya kuanza rasmi kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.
Baadhi ya wasanii ambao ni mabalozi wa Maziwa ya ASAS wakiwa katika uwanja wa Samora kwa ajili ya kushuhudia mtanange huo.