Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Leonard Chamriho akikata utepe pamoja na Dk. Omary Mbura Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL na Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la ATCL Mhandisi Ladslaus Matindi wakikata utepe kama ishara ya uzinduzi rasmi wa safari za ndege za shirika hilo kutoka Dar es salaam Tanzania kwenda katika jiji la Guangzhou nchini China ambazo zimezinduliwa Mei 08, 2021 kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JNIA Teminal III jijini Dar es salaam.
Shirika hilo litafanya safari zake mara moja kwa wiki mbili na kadiri litakavyotimiza masharti ya Usafiri wa Anga nchini humo yaliyowekwa na mamlaka kuhusu ugonjwa wa Corona (UVICO19) litaongezewa safari kulingana na mamlaka zitakavyoona.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-DAR ES SALAAM)
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Leonard Chamriho akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Ndege la ATCL kabla ya ndege hiyo kuanza safari yake kuelekea nchini China wakati shirika hilo lilipozindua rasmi safari zake jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Leonard Chamriho akiwahutubia wageni waalikwa mbalimbali kabla ya kuzindua safari hizo, Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ATCL Injinia Ladslaus Matindi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ATCL Injinia Ladslaus Matindi akimkaribisha Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Injinia Leornald Chamriho ili kuzindua rasmi safari hizo.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Leonard Chamriho akikata keki katika hafla hiyo huku watendaji wa Shirika la Ndege la ATCL na baadhi ya wafanyakazi wakipiga makofi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Ndege la ATCL wakiwa katika hafla hiyo ya uzinduzi.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Leonard Chamriho akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Shirika hilo mara baada ya uzinduzi huo.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Leonard Chamriho akikata utepe pamoja na Dk. Omary Mbura Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL na Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la ATCL Mhandisi Ladslaus Matindi wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kwenye ndege.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Leonard Chamriho akikata utepe pamoja na Dk. Omary Mbura Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL na Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la ATCL Mhandisi Ladslaus Matindi wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo.
Baadhi ya picha zikionesha abiria wakiingia kwenye ndege ya ATCL tayari kwa kuelekea Guangzhou nchini China.
Paadhi ya abiria wakiwa wameketi kwenye viti wakisubiri taratibu zote zimakilike tayari kwa kuanza kwasafari hiyo.
Abiria mbalimbali wakijiandaa kuingia kwenye ndege tayari kwa kunza safari ya kwenda Guangzhou Nchini China usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa ndege wa JNIA jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa shirika la ndege la ATCL wakiwa katika hafla hiyo.
Ndege za shirika la ndege la ATCL zikiwazimeegeshwa Terminal III kwa ajili ya kupakia abiria.