Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Francis Masanja akijibu swali la Mhe. Innocent Sebba Bilakwate wakati wa mkutano wa 3 Kikao cha 5 cha Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mapema leo Aprili 08, 2021 Jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………………
Serikali imetenga shilingi milioni 311.9 zitakazotumika kuchonga Barabara yenye urefu wa kilometa 20 katika hifadhi ya Taifa Rumanyika karagwe na kilometa 51 katika Hifadhi ya Taifa ya Ibanda Kyerwa katika mwaka wa fedha 2020/2021.
Akijibu Swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro ,Mhe. Masanja ameeleza kuwa hifadhi za Taifa za Ibanda Kyerwa na Rumanyika karagwe zilianzishwa kupitia tangazo la Serikali Na 509 na 510 la tarehe 5/7/2019 .
Amesema hifadhi hizo zilitokana na kupandishwa hadhi kwa yaliyokuwa mapori ya akiba ya Ibanda na Rumanyika .
“Ili kuwezesha hifadhi hifadhi hizo kufikika kwa urahisi Serikali kupitia TANROADS na TARURA iliyokuwa ikitengeneza Barabara mbalimbali zinazorahisha kufika kwa watalii katika hifadhi hizo , Barabara hizo ni pamoja Mgamkorongo iliyopo wilaya ya korogwe hadi murongo wilayani Kyerwa yenye urefu wa kilometa 112 ambayo inafanyiwa matengenezo na TANROADS kila mwaka na imewekwa katika mpango wa Kujengwa kwa kiwango cha lami katika mwaka wa fedha 2020/2021” Amesisitiza Mhe.Mary Masanja.
Aidha, amesema jitihada hizo za kuboresha miundombinu ya Barabara katika hifadhi ya Taifa Ibanda Kyerwa na Rumanyika Karagwe na maeneo mengine yote ya hifadhi zitasaidia kuweka Mazingira mazuri yatakayowezesha hifadhi hizo kutembelewa na watalii wengi wa maeneo ya karibu pamoja na wageni kutoka nchi jirani.
Kuhusu ulinzi wa maeneo hayo ameeleza kuwa wizara imekuwa ikiyaanisha maeneo yote na kuweka mipaka.
” Katika hifadhi ya Ibanda Kyerwa na Rumanyika tulifanya tathmini baada ya wataalamu wetu kuainisha mipaka, utekelezaji wake tunaendelea nao kwa kuandaa Mazingira ya kuwapeleka wataalamu kwa ajili ya gharama za uthamini na kuanisha maeneo ambayo yanachangamoto za uhifadhi ” Amesisitiza.