Home Mchanganyiko RUNGWE YAOMBA KANUNI NA MIONGOZO YA KUKASIMISHWA MAJUKUMU YA TBS

RUNGWE YAOMBA KANUNI NA MIONGOZO YA KUKASIMISHWA MAJUKUMU YA TBS

0

Mkaguzi wa TBS Mhandisi Yekonia Sanga ( kulia) akimkabidhi cheti cha usajili Meneja wa Hoteli ya Landmark,Tukuyu mkoani Mbeya Bw. Razack Godfrey (kushoto), mara baada ya kukamilisha usajili kwa njia ya mtandao Mbali na usajili, hoteli hiyo ilikaguliwa eneo la kuandalia, hifadhia na kulia chakula ili kujiridhisha na usalama wake.

Mkaguzi wa TBS, Bw. Peter Namaumbo (kushoto) akimpa maelekezo muuzaji wa duka la vipodozi Bi. Sarah Marere(kulia) kuhusu utaratibu wa kusajili bidhaa hizo, alipotembelewa mapema leo katika duka lake lililopo kituo cha mabasi Tukuyu wilayani Rungwe.

……………………………………

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bi. Loena Peter ameliomba Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kufuatilia kwa karibu kanuni na miongozo itakayowezesha halmashauri kukasimishwa majukumu ya TBS na
kutekeleza jukumu hilo kwa ukamilifu. Bi. Loena ameyasema hayo mapema leo alipotembelewa na maafisa wa TBS kanda ya Nyanda za juu Kusini, Mhandisi Yekonia Sanga (kushoto) na Bw. Peter Namaumbo (kulia) kwa lengo la kujitambulisha kabla ya kuanza ukaguzi wa bidhaa sokoni na usajili wa majengo ya bidhaa za vyakula na vipodozi wilayani hapa.