……………………………………………………………………………………….
Taasisi ya ushirika wa wadau wa mifumo ya kuboresha mifumo ya masoko nchini (AMDT) imewakutanisha wadau wa kilimo ikiwa ni wakulima, wafanyabiashara wa zao la alizeti, Wizara za kisekta na taasisi za mabenki na kutoa mafunzo kwa wakulima wanawake na vijana kutambua fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo hicho.
Sambamba na kuwashirikisha wakulima wanawake na vijana kulima kwa tija na kuongeza thamani ya mazao katika mnyololo wa thamani ili kushindana katika soko.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya semina hiyo afisa mtendaji wa Taasisi hiyo bw. Charles Ogutu, amesema kuwa sekta ya kilimo nchini inajumuisha theruthi mbili ya watanzania lakini mchango wake katika pato la taifa bado kidogo sana.
“Tunataka kuwafundisha wanawake pamoja na vijana kwakua wao ndiyo kundi kubwa katika taifa letu kama watafanikiwa kutambua fursa zilizopo kwenye sekta hii ya kilimo basi taifa litapiga hatua wanawake siku zote ukiwafundisha kitu wanafanya vizuri sana kuliko wanaume” amesema Ogutu.
Bwana Ogutu amebainisha kuwa wanawake na vijana hawatakiwi kuendelea kushiriki katika kilimo kimazoea bali wabadilike katika mitazamo yao ambapo wataweza kulima kwa tija na kujikwamua kiuchumi” amesema.
Amesema kuwa ili kufikia Tanzania ya viwanda kilimo kinatakiwa kupatiwa kipaumbele na kundi kubwa litakalofanikisha hali hiyo ni vijana na wanawake.
“Vijana ndiyo wenye nguvu na ndiyo idadi kubwa katika taifa hata teknolojia hizi za kisasa wao wanaweza kuzitumia ipasavyo hivyo kwa kuwapatia elimu ya kutambua fursa zilizopo kutafanikisha kufikia malengo yao” amesema.
Kwa upande wake Bi. Theodora Pius, kutoka mtanadao wa vikundi vya wakulima wadogo (MVIWATA) amesema kuwa matatizo makubwa ya wakulima nchini ni pamoja na upatikanaji wa masoko ya uhakika ya mazao yao na ardhi.
Nae mjumbe wa Bodi ya Chama cha wanawakae wafanyabiasahra nchini (TWCC) Victoria Mwanokuzi, amebainisha kuwa wanawake wengi wamekuwa wakishindwa kutokana na kukosa elimu kuhusu mambo mbalimbali.
Ameongeza kuwa “Wanawake wengi walikuwa wanalalamika kuhusu mitaji lakini tumewaeleza sisi kama chama cha wafanyabiashra wanawake nchini tumeingia mkataba na benki ya NMB na CRDB hivyo wanaweza kupata mikopo yenye riba ya asilimia 14”, amesema.
Meneja wa Tawi la CRDB, tawi la chuo kikuu cha UDOM Ditrick Mdoe amesema wao kama taasisi ya fedha wamekuwa wakitoa mikopo kwa ajili ya wakulima na wasindikaji wa mazao ya kilimo kama vile alizeti.
“Katika hili changamoto tunazaokutana nazo ni wakulima kushindwa kufanya mambo yao ndani ya muda hivyo wakati mwingine kuchukua mikopo wakiwa wamepishana na msimu wa mazao hivyo leo tumewaelimisha muda gani sahihi kwao”amesema Mdoe