Country Director Repssi Tanzania Bi. Edwicic Mapalala akizungumza jambo leo jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya Ustawi wa Jamii Duniani yaliondaliwa na Taasisi ya Raising Up Friendndiship Foundation kwa kushirikiana na mtaalam wa ustawi wa jamii Bi. Joyce Makate.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Raising Up Friendndiship Foundation, Bi. Hilda Ngasa akizungumza jambo jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya Ustawi wa Jamii Duniani.
Mtaalam wa Ustawi wa Jamii Bi. Joyce Makeka akizungumza jambo jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya Ustawi wa Jamii Duniani.
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Wafanyakazi wa Ustawi wa Jamii Tanzania (TASWO) Bi. Epheta Msiga.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Guardian Angels Bi. Miriam Msangi.
****************************************
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Wazazi na walezi wametakiwa kuwa karibu na familia zao kwa kutenga muda wa kuwaangalia watoto jambo ambalo litasaidia kuwaepusha kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji ambavyo vimeonekana vikiongezeka katika jamii.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya Ustawi wa Jamii Duniani yaliondaliwa Taasisi ya Raising Up Friendndiship Foundation kwa kushirikiana na mtaalam wa ustawi wa jamii Bi. Joyce Makate, Country Director Repssi Tanzania Bi. Edwicic Mapalala, amesema kuwa wazazi wanatakiwa kuwajibika kwa kuangalia familia zao.
Bi.Mapalala ni mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yaliowakutanisha wataalam wa ustawi wa jamii kutoka taasisi mbalimbali, amesema kuwa wakati umefika wa kuwekeza katika jamii kwa kutoa elimu ambayo itasaidia kuondoa vitendo vya udhalilishaji.
“Ukatili unaongezeka kwa watoto, hii inatokana na baadhi ya wazazi hawana muda wa kufatilia familia zao, muda mwingi wapo katika majukumu ya kikazi, hivyo wanatakiwa kubadilika na kutenga muda wa kuongeza na watoto kila siku wanaporudi nyumbani ” amesema Bi. Mapalala.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Raising Up Friendndiship Foundation, Bi. Hilda Ngasa, amesema kuwa taasisi na wadau mbalimbali wanatakiwa kushirikiana katika kutokomeza ukatili.
Bi. Ngasa amesema kuwa kusaidia ni jambo la muhimu ili kuhakikisha malengo husika yaliokusudiwa yanafikiwa katika nyanja mbalimbali katika jamii.
”Tuwashirikishe vijana wetu katika familia kwa kuwaelimisha, jamba ambalo litasaidia kuondokana na tatizo la ukatili” amesema Bi. Ngasa.
Mtaalam wa Ustawi wa Jamii Bi. Joyce Makeka, amesema kuwa wakati umefika jamii kubadilika kwa kujiepusha kufanya vitendo ambavyo sio rafiki kwa jamii.
Bi. Makeka ameeleza kuwa asilimia kubwa watoto wanafanyiwa ukatili kisaikolojia na ngono, jambo ambalo jamii kwa pamoja inatakiwa kuungana na kulipiga vita.
“Malezi ni huduma ya msingi kwa watoto ambayo yatawasaidia kuwaleta pamoja na kuwa karibu na wazazi katika kuwashirikisha kila jambo” amesema Bi. Makeka.
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Wafanyakazi wa Ustawi wa Jamii Tanzania (TASWO) Bi. Epheta Msiga, amebainisha kuna changamoto nyingi katika utekelezaji wa majukumu ya kupinga ukatili jambo la muhimu ni ushirikiano na kusaidiani ili kufikia lengo.
Hata hivyo amempongeza Mkurugenzi wa Taasisi ya Raising Up Friendndiship Foundation, Bi. Ngasa kwa mwamko wake katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake ikiwemo kupiga ukatili wa kijinsia kwa watoto.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Guardian Angels Bi. Miriam Msangi, amesema kuwa taasisi yake imekuwa ikiwasaidia watoto wenye uhitaji kwa muda wa mwaka mmoja ili waweze kuwafikia watoto wengi zaidi.
Bi. Msangi ameeleza kuwa licha kutoa msaada kwa muda wa mwaka mmoja, wemekuwa na utamaduni wa kuendelea kuwasaidia watoto kwa kuwawezesha walezi wao ili waweze kuishi katika mazingira rafiki.
“Wakati umefika kwa wadau na taasisi mbalimbali kushikamana kwa pamoja tuweze kushirikiana kwa kila jambo” amesema Bi. Msangi.
Katika maadhimisho hayo ya siku ya Ustawi wa Jamii Duniani kauli mbinu ni Ubuntu, ambapo imelenga kuhamasisha usawa, umoja na ushirikiano katika kufanisha masuala mbalimbali ya jamii kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa.