Mahindi ya njano
Na Richard Mwaikenda, Dodoma.
Wizara ya Kilimo, imelitafutia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), soko la mahindi ya njano tani milioni moja Misri.
Neema hiyo ya soko la mahindi ya njano, imetangazwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Gerald Kusaya katika hafla ya kutiliana sahihi mkataba wa ushirikiano katika sekta ya kilimo iliyofanyika hivi karibuni Makao Makuu ya jeshi hilo, wilayani Chamwino, Dodoma.
Amesema moja ya mambo watakayoshirikiana na JKT ni kuwatafutia masoko ya mazao kabla ya hata kuanza kuzalisha ili kuwa na uhakika ya kuyauza, hivyo ameihimiza JKT kaunza haraka kulima zao hilo ili kukidhi soko hilo.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Kusaya akielezea kuhusu soko hilo…