Klabu ya kuogelea ya Bluefins imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Taliss baada ya kukusanya pointinyingi zaidi ya klabu nyingine tano zilizoshiriki.Klabu hiyoimepata jumla ya pointi 1,619 katika katika mashindano yaliyofanyika kwenyebwawa la kuogelea la klabu ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam.
Kati ya pointi hizo, 872 zilipatikana kwa upande wa wanaume na 747 kwa upande wa wanawake.Klabu ya Dares Salaam Swimming Club illishinda nafasi ya pili kwa kupata jumla ya pointi 1,592.5na waandaaji wa mashindano hayo, Taliss walishinda nafasi ya tatu kwa kupatapointi 1,308.
Klabu ya Mwanza (MSC) ilimaliza katika nafasi yanne kwa kupata pointi 954 na FK BlueMarlins ikishika nafasi ya tano kwa kupata pointi 854.
Timu ya Morogoro (MisPiranhas) ilishika nafasi ya sita baada ya kujikusanyia pointi 595.Katikamashindano hayo, klabu ya Bluefins ilishinda jumla ya medali 52 ambapo kati yahizo, 24 ni dhahabu, 11 fedha na 17 shaba.
Muogeleaji mwenye umri wa miaka 10,Maryam Ipilinga ailiweza kuvuna pointi nyingi zaidi kwa klabu hiyo baada yakujikusanyia pointi 115 baada yakushinda medali tano za dhahabu.
Muogeleajihuyo alifuatiwa na Aminaz Kachra (11) aliyevuna pointi 109 kwa kushinda medalitatu za dhababu na mbili za fedha huku Lina Goyayi (11) alivuna pointi 100 kwa kushinda medali mbili za dhahabu na mojaya shaba.Piamuogeleaji Gervas Sayi (8) aliipatia timu yake pointi 100 kwa kupata medali zatano za dhababu.
Waogeleaji wengine wa klabu hiyo waliofanya vizuri ni AaronAkwenda aliyeshinda dhababu mbili na shaba mbili, Filbertha Demello (dhahabu,fedha na shaba tatu), Christian Fernandes (dhahabu, shaba tatu), Muskan Gaikwad(fedha na shaba), Sahal Harunani shaba mbili) na Delbert Ipilinga ambaye ameshindamedali za fedha tatu.Pia kunaAvinav Mahapatra ( 2 dhahabu, fedga nashaba), Mohamed Manji (shaba), Sarah Shariff (2 dhababu, fedha na shaba) na Aaliya Takim ameshindamedali moja ya shaba.
captionWaogeaji wa klabu ya Bluefins wakiwa na medali zao baada ya kushinda mashindano ya Taliss.