Ernest Mintah Mkurugenzi wa Shirikisho la wadau wa Korosho Afrika (African Cashiew Alliance) akizungumza katikia mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam mkutano huo ulizungumzia maandalizi ya mkutano wa wadau wa zao la Korosho utakaofanyika nchini kuanzia tarehe 7-9 mwezi Nomvemba kutoka kulia ni Francis Alfred kutoka Bodi ya Korosho Tanzania na Dk. Steven Ngailo kutoka Wizara ya Kilimo na Chakula.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
……………………………………………..
Shirikisho la Korosho Afrika (ACA) litakuwa wenyeji wa Mkutano wa 13 wa Korosho na Maonesho kuanzia tarehe 7-9 Novemba 2019 jijini Dar es Salaam, Tanzania katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).
Mada ya mkutano wa mwaka huu ni “Kuendeleza Ushirikiano, Kushawishi Mabadiliko katika Soko”. Lengo la mwaka huu ni kuchambua mabadiliko ya sasa ya soko, mwitikio wa serikali na watendaji wa mnyororo wa thamani na kuchanganua wajibu wa wadau wote wa umma na binafsi katika kushughulikia masuala yanayojitokeza.
Kwa miaka mingi, Mkutano wa Mwaka wa Korosho wa ACA umekuwa ni tukio kubwa sana la korosho Afrika, likiwakutanisha pamoja wadau wa tasnia mbalimbali za korosho kutoka duniani kote. Kwa siku tatu za kusisimua, wakulima, wafanyabiashara, wabanguaji, wasafirishaji, viongozi wa serikali, watengenezaji wa vifaa, na watoa huduma watakutana ili kuzungumza na kujadili mwelekeo wa tasnia, fursa na changamoto.
Mwaka 2008, Tanzania ilifanikisha kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Mwaka wa Korosho wa ACA na sasa baada ya miaka kumi hatimaye mkutano unarudishwa tena nchini. Tanzania inazalisha kiasi cha 313,000MT za korosho mbichi katika msimu wake wa 2017/18 na kwa sasa, baada ya Cote d’Ivoire, ni mzalishaji mkubwa wa pili wa korosho Afrika. Pia, mwaka 2017, korosho ziliizidi tumbaku kwa kuwa zao la Tanzania linalosafirishwa nje kwa wingi, likiingiza mapato zaidi ya mapato yanayounganishwa kutokana na kahawa, pamba, chai, karafuu na katani.
Korosho ziliingiza Dola za Marekani milioni 575.6 mwaka 2018, zikiongezeka kutoka Dola milioni 340 mwaka 2017. Wakiamini katika mustakabali wa sekta ya korosho Afrika, na kuendelea kukua kwa sekta ya korosho na uchumi wa Tanzania, Bodi na Menejimenti ya ACA, kwa kushauriana na sekta binafsi, wameichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wake wa mwaka wa korosho wa 2019!
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Korosho wa ACA unafanyika kwa ushirikiano wa ofisi za serikali ya Tanzania zinazosimamia sera zinazohusiana na korosho nchini Tanzania, ambazo ni Wizara ya Kilimo, Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania.
Mkutano unatumika kama fursa ya kipekee kwa wadau wa Afrika na wa kimataifa kukutana na kujadili kuhusu tasnia ya korosho Afrika, ambayo inalima zaidi ya asilimia 56 ya korosho inayosambazwa duniani kote. Afrika ni mzalishaji mkubwa wa kanda na muhimu sana katika mnyororo wa thamani wa faida na uzalishaji duniani!
Mkutano wa mwaka huu utalenga katika mada muhimu kama vile utungaji sera na changamoto za sekta ya korosho katika utekelezaji wake, ubunifu wa ubanguaji, utafiti wa uzalishaji, upataikanaji wa fedha, uwekezaji katika tasnia ya korosho Afrika, usalama wa chakula na kanuni za maadili pamoja na kuboresha mifumo ya taarifa za masoko.
Ratiba ya siku tatu itahusisha watendani mbalimbali wa nchini na wa kimataifa katika tasnia ili kuhakikisha kwamba tasnia ya korosho Afrika inabakia kuwa mchangiaji anayeonekana ndani ya sekta. Mwisho, mkutano utafungwa kwa kuchagua ziara za mapumziko & kujifunza ambapo washiriki wanaweza kutembelea ama uzalishaji/ubanguaji wa korosho karibu na Dar es Salaam au kisiwa cha Zanzibar.
Tunawakaribisha katika mkutano wetu ili kuungana na washiriki na kujadili mustakabali wa tasnia ya korosho Afrika – Tutaonana Novemba mwaka huu jijini Dar es Salaam!