Meneja wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA Kanda ya Ziwa Sophia Mziray akielezea kuhusu wanavyodhibiti Dawa na Vifaa tiba vinapotengenezwa au kuingizwa nchini na kwenye masoko
Ofisi ya Mamlaka ya Dwa na Vifaa Tiba Kanda ya Ziwa.
…………………………………………………
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa imesema inafanya kazi ya kudhibiti wa Dawa na Vifaa Tiba ikiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata Dawa na Vifaa vyenye ubora,Usalama na Ufanisi.
Imesema kuwa imekuwa na ufatiliaji dawa katika mnyororo mzima wakati inaingia na wakati usambazi kutoka chanzo Kikuu na kwenda kwa watumiaji.
Hata hivyo amesema wafanyabiasha wafuate taratibu kwani hawawezi kupitisha dawa na ikaendelea kuumiza wananchi wamejipanga kila sehemu ya mipaka ili khakikishakila kitu kinakwenda sawa.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika Ofisi za Kanda ya Ziwa hivi karbuni Meneja Meneja wa TMDA Sofia Mziray Kanda hiyo amesema kuwa udhibiti wa Dawa na Vifaa Tiba unahitaji ushirikiano na wadau mbalimbali kwani madhara yatokanayo na Dawa wakati kunapotokea tatizo hayawezi kugusa mtu mmoja Bali yatagusa watu wote kutokana dawa ilivyosambaa.
Amesema Kanda ya Ziwa ina Mikoa Sita pamoja na mipaka ya nchi zilizo katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo bila kuwa na utaratibu wa kufuatilia uingizaji wa Dawa kunaweza kutoa mwanya kwa wafanyabiashara kuingiza dawa bandia ,au zilizoisha muda na kuleta madhara katika jamii.
Mziray amesema kutokana na Ofisi ya Kanda ya Ziwa kuwa Mwanza wameweza kusogeza huduma Bariadi mkoani Simiyu ambapo watahudumia Mikoa ya Kanda ya Ziwa Mashariki.
Amesema wamekuwa na ukaguzi aina tofauti ukiwemo ukaguzi elekezi wa majengo mapya ya kutengenezea dawa ,Uhifadhi wa dawa ,Vifaa Tiba pamoja na vitendanishi kwa kutoa ushauri wa kitaalam kabla kuanza uzalishaji.
Amesema pia kuna ukaguzi wa kawaida katika kujihakikishia kuwa bidhaa zinaendelea kuzalishwa ,kuhifadhiwa kwa kutoa utaratibu zikiwa na ubora,salama na zenye ufanisi.