Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael akifunga Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji wa Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala na Utoaji wa taarifa Barani Afrika iliyomalizika leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael akimsikilza Mwakilishi wa Kurugenzi inayoshughulikia Masuala ya Siasa Umoja wa Afrika, Bw. Issaka Garba Abdou wakati wa kufunga Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji wa Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala na Utoaji wa taarifa Barani Afrika, iliyomalizika leo jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa Semina ya Kuzijengea Uwezo Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuhusu Utekelezaji wa Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala na Utoaji wa taarifa Barani Afrika wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael alipokuwa akifunga semina hiyo jijini Dar es Salaam.