Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akiongoza zoezi la
maadhimisho ya uzinduzi wa upandaji miti kitaifa kwa ngazi ya wilaya mkoani
Singida hivi karibuni.
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi akishiriki zoezi
hilo kikamilifu.
wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo (kulia)na Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi kwa pamoja wakiwajibika kwenye
maadhimisho hayo.
Mkuu wa Idara ya Usafishaji na Mazingira, Halmashauri ya
Wilaya ya Ikungi, Onesmo Rwehumbiza akipanda mti.
wa Kata ya Dung’unyi Yahaya Njiku na Kamanda wa Jeshi la Akiba wilaya ya Ikungi
Massawe wakishiriki zoezi hilo.
wa Jeshi la Akiba wakisikiliza hotuba ya DC Mpogolo kabla ya kuanza zoezi la
kupanda miti kwenye maadhimisho hayo.
wa Vitengo na Idara mbalimbali wakisikiliza hotuba ya DC Mpogolo kabla ya
kuanza zoezi la kupanda miti kwenye maadhimisho hayo .
ya uzinduzi wa upandaji miti yakiendelea.
ya uzinduzi wa upandaji miti yakiendelea.
ya uzinduzi wa upandaji miti yakiendelea.
ikiendelea.
ikiendelea.
wa Wilaya ya Ikungi akishiriki ipasavyo zoezi hilo..
Misitu wa TFS kutoka Wilaya ya Ikungi, Wilson Pikoloti akishiriki maadhimisho
hayo.
Mwonekano wa mradi wa ujenzi unaoendelea wa Majengo ya
itakayokuwa Hospitali ya Wilaya ya Ikungi.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani hapa, Edward Mpogolo
ameongoza mamia ya watumishi katika maadhimisho ya uzinduzi wa upandaji miti
kiwilaya, ikiwa ni safari ya mwendelezo wa shabaha iliyopo ya hitaji la
kufikisha idadi ya miti isiyopungua 709,000, huku kila kaya ikitarajia kupanda
miti 10 kwa msimu wa 2020/2021.
Katika uzinduzi huo uliofanyika hivi karibuni, jumla ya
miche ya miti 400 ilipandwa eneo la kijiji cha Muungano, mahali unapotekelezwa
mradi wa ujenzi wa majengo ya itakayokuwa hospitali ya Wilaya ya Ikungi, huku
miti mingine takribani elfu 30 inayozalishwa na TFS ikitarajiwa kusambazwa na
kupandwa kwenye taasisi nyingine zote ndani ya wilaya hiyo.
“Shabaha yetu kwa mwaka huu kwanza ni kupanda zaidi ya miche
laki saba lakini pia tunatarajia kupanda zaidi ya miche ya korosho milioni
moja. Na kuhusu miche ya korosho tayari Jeshi la Kujenga Taifa hapa wilayani
wameshazalisha zaidi ya miche laki 3…kikubwa tuendelee kuhamasishana,” alisema
Mpogolo
Aidha, aliwataka wakazi wanaoishi ndani ya wilaya hiyo
kuhakikisha idadi iliyopangwa ya kupanda miti 10 kwa kila kaya inatekelezwa
kikamilifu kwa kiwango cha kuchanganya aina mbalimbali za miti ikiwemo ile ya
mbao, lakini bila kusahau kupanda nje ya nyumba zao miti ya kivuli, miembe,
korosho na palachichi.
Hata hivyo, aliwataka TFS kuongeza idadi ya uzalishaji miche
kutoka elfu 30 iliyopo kwa sasa na kufikia angalau elfu 50 ili kukidhi hitaji
la miti hiyo kwa kuzingatia jiografia ya ukubwa wa maeneo yanayozunguka wilaya
hiyo ikiwa ni kubariki jitihada zinazoendelea katika kukabiliana na ukame.
“Kwa mwaka huu sitarajii tena kuona kuna upotevu wa miti, nikuombe
Mkurugenzi tusimamie kikamilifu sheria zetu ndogondogo ili kutunza hii miti
ambayo tumeanza kuipanda leo na tutakayoendelea kuipanda kwa mwaka mzima.
Msiruhusu mifugo iwe sababu ya upotevu wa miti yetu,” alisema Mpogolo na
kuongeza:
“Tumeamua kufanya uzinduzi huu kwenye hospitali hii sababu
tunataka wagonjwa wetu wanapofika hapa wapumzike vizuri na wapate kivuli na
hewa safi. Rais John Magufuli ametupatia jumla ya shilingi bilioni 1.5 kwa
ajili ya ujenzi wa majengo haya ya hospitali yetu ya wilaya…tunataka siku akija
kuizindua basi akute kuna mazingira rafiki na uoto wa miti ya kutosha.”
Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wilaya aliagiza
kuhakikisha wale wote waliovamia maeneo ya misitu ya Minyughe na Mlilii
wanaondoka mara moja ili kuokoa bionuai za misitu hiyo iliyopo ndani ya wilaya
ya Ikungi, ambayo siku hadi siku imeendelea kuathiriwa na uvamizi huo unaenda
sambamba na shughuli za kibinadamu.
“Kwa bahati nzuri TFS kwa kushirikiana na Halmashauri wameanza
kutenga baadhi ya maeneo na tumeshaanza kuangalia athari zilizojitokeza kwenye
misitu hiyo ili kukamilisha taratibu zote kuwezesha msitu kupimwa na kupata GN
ili tuweze kuumiliki kisheria,” alisema.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ikungi Justice
Kijazi alisema uoto wan chi yetu ni kitu muhimu na ili tuweze kurithisha uoto
huo kwenye kizazi kinachokuja tunapaswa kutengeneza mazingira mazuri ya
upandaji miti kama zoezi endelevu kwa mfano wa tukio la uzinduzi huo.
Alisema kwa Halmashauri ya Ikungi kuanzia mwaka 2016/2020
imefanikiwa kupanda miti 1,385,900 lakini kati ya hiyo iliyopona mpaka sasa ni
145,860 sawa na asilimia 63.
“Tatizo kubwa linalosababisha uharibifu wa miti inayopandwa
ni mifugo inayozunguka kwenye maeneo yetu. Natambua mifugo ni neema lakini
wengi wetu tunaifuga kiholela,” alisema Kijazi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Usafishaji na Mazingira,
Halmashauri ya Ikungi, Onesmo Rwehumbiza, alimweleza Mkuu wa Wilaya kwamba kuna
misitu miwili ya asili ya Hifadhi, yaani Miili na Minyughe, lakini misitu hii
kwa sasa imevamiwa na watu zaidi ya 1200 kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje
ya wilaya ya ikungi.
“Pamoja na halmashauri ya wilaya kujitahidi kuweka mabango
ya kukataza mtu yeyote kuingia kwenye hifadhi hizo lakini bado wananchi
wanakaidi agizo hilo kwa kuendelea kuingia hifadhini na kufanya uharibifu
mkubwa kwenye misitu hiyo ya asili,” alisema Rwehumbiza.