Picha ni Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, akizungumza
na Management ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na Wahandisi wa
Umwagiliaji wa Mikoa hawapo pichani, katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo
Uliyopo jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kushoto, akifuatilia taarifa
inayowasilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
Bw. Daudi Kaali (kulia) katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi
wa Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bi. Mary Mwangisa
akizungumza kabla ya kuanza kwa kikao kazi na NaibuWaziri wa Kilimo
Mhe. Hussein Bashe katika ukumbi wa Wizara ya KilimoJijiniDadoma
Picha ikionesha baadhi ya Wahandisi wa Umwagiliaji wa Mikoani chini
wakishiriki katika kikao kazi kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Kilimo
Hussein Bashe jijini Dodoma
Picha kionesha baadhi ya watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Hussein Bashe katika
kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mapema
Na Mwandishi Wetu – Dodoma.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, Ameitaka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, kutumia wataalamu na rasilimali za ndani katika kazi za upembuzi yakinifu katika ujenzi wa Miundombinu ya Umwagiliaji,ili kupunguza gharama za ujenzi wa miradi ya miundombinu hiyo.
Bashe aliliyasema hayo Jijini Dodoma alipokutana na Management ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na Wahandisi wa Umwagiliaji nchini nakuagiza Mitambo 56 inayomilikiwa na Tume popote ilipo nchini ikaguliwe nakufanyiwa matengenezo huko iliko na yenye hali mbaya iletwe katika ofisi za makao makuu ya Tume jijini Dodoma kwa matengezo zaidi.
Sambamba na hilo aliagiza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ifanye Utaratibu wa kuyutambua maeneo yote ya kilimo cha umwagiliaji nchini yapo wapi yana ukubwa gani na yanalima mazao gani ilikuweza kujua ni maeneo gani yanayoweza kufanyiwa maboresho na kumwagiliwa kihalisia.
Naibu Waziri Bashe aliwashauri wataalamu hao, kuweza kuona namnayakuhusisha sekta binafsi katika kuboresha miundombinu ya umwagiliaji na kuanzisha kilimo Biashara kupitia sekta ya umwagiliaji, pamoja, nakuwaagiza kuainisha eneo litakalotumika kwa kilimo cha umwagiliaji katika Bwawa la mwalimu Nyerere, nakuliwekea mipaka ili lisiweze kuvamiwa na shughuli nyingine za kibinadamu.
Aidha, Naibu Waziri Bashe ameiagiza Tume hiyo iwe na mpango mkakati wa miaka mitano wautekelezajiwa kuongeza eneo la Umwagiliaji, lenye ukubwa wa Hekta milioni moja sambamba na hilo kuangalia litazalisha mazoa ya aina gani, kwa kiasi gani litakuwa katika vijiji gani na litatumiwa na wakulima wangapi.
“Pamoja na hili mkaena Tasisi ya kuzalisha Mbegu (ASA), Taasisi ya Tafiti ya Mazao ya Kilimo (TARI) ili katika eneo hilo kuweza kutenga walau asilimia ishirini 20% ya eneo kwa ajili ya kuzalisha mbegu”.Alisisitiza.
Naibu Waziri Bashe, Aliitaka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Ifanye ukarabari wa mundombinu ya Umwagiliaji katika skimu kwa kuwwashirikisha wakulima.