***********************************
Kikosi cha wachezaji 23 wa Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC kitaondoka jioni ya leo kuelekea Jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Januari mbili katika uwanja wa Sokoine.
Aidha katika msafara huo pia utahusisha benchi la ufundi pamoja na viongozi wa tano wa Timu hiyo .
KMC FC itacheza mchezo huo wa raundi ya 18 katika mzunguko wa pili ambapo katika mzunguko wa kwanza iliweza kuifunga Timu hiyo mabao manne kwa sifuri katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Aidha kuhusu hali za wachezaji, wapo katika hali na morali nzuri itakayo wezesha kupata matokeo mazuri ikiwa ni pamoja na kupata alama tatu muhimu ugenini dhidi ya wapinzani Mbeya City.
Hata hivyo kabla ya kuondoka, wachezaji hao wamefanya mazoezi mepesi asubuhi ya leo ikiwa ni katika mkakati wa kujiweka vizuri kuelekea kwenye mchezo huo.
Imetolewa na Christina Mwagala
Afisa Habari na Mahusiano wa Timu ya KMC FC