TAARIFA KWA UMMA

Kufuatia taarifa hii inayosambazwa katika Mitandao ya Kijamii, Jeshi la Polisi lingependa kutoa ufafanuzi kulingana na ushahidi uliokusanywa kupitia kwa watu mbalimbali na kupitia uchunguzi wa kisayansi uliokwisha fanyika hadi sasa.

 Ni kweli kwamba taarifa za kupotea kwa Vincent Peter Massawe zilifikishwa Kituo cha Polisi Kigamboni tarehe 19.11.2024 na Mke wake na upelelezi ulianza  mara moja  na kuthibitisha kuwa  ni kweli alikuwa na harusi tarehe 16.11.2024 na bàada ya harusi alitafuta gari yakuwarejesha ndugu zake na wageni wengine Moshi Mkoani Kilimanjaro.

 Aidha, ushahidi mwingine uliopatikana ni kwamba wakati wa maandalizi aliazima gari kutoka kwa jamaa yake ili imsaidie katika shughuli za harusi  yenye namba T.642 EGU aina ya Toyota Ractis.

 Baada ya harusi hakurejesha gari hiyo kwa mwenyewe badala yake tarehe 18.11.2024 ambayo inadaiwa alikuwa anafuatiliwa na gari ambayo alikuwa anaitilia mashaka ndiyo siku hiyo hiyo aliuza gari hiyo kwa kiasi cha shilingi milioni tisa (9) akalipwa shilingi milioni nane ( 8) ikabaki milioni moja (1). Taarifa iliyopo inaonyesha kuwa siku hiyo hiyo alimtumia mke wake kiasi cha fedha ili alipe madeni mengine yaliyotokana  na harusi ikiwepo coaster aliyokodisha kuwarejesha wageni wake Moshi.

 Gari hilo aina ya Toyota Ractis limefuatiliwa  na limekamtwa.

 Aidha, ushahidi mwingine unaonyesha huyu Vincent Peter Massawe, pia anadaiwa na watu wengine wawili mmoja kiasi cha shilingi milioni hamsini na tatu (53) na mwingine shilingi milioni kumi na sita (16).

 Ukweli wa tukio hili utafahamika muda si mrefu kama amejipoteza au la kulingana na mtiririko wa ushahidi ulivyo na hili linategemea  hasa tukipata ukweli kutokà kwa mke wake kwani inadaiwa anao ufahamu mkubwa wa jambo hili. Mwisho Umma utajulishwa taarifa zilizo sahihi kuhusu Bwana Peter Vicent Masawe.

                                                          Imetolewa na:                                                              

David A. Misime – DCP

Msemaji wa Jeshi la Polisi

Makao Makuu ya Polisi

                                                                                                                Dodoma, Tanzania