Picha mbalimbali kutoka katika Mkutano wa 10 wa Tathmini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, unaofanyika katika Ukumbi wa Mabeyo jijini Dodoma.

Mkutano huo wenye kaulimbiu isemayo “Lishe Bora, Uchumi Imara, Tabasamu kwa Wote” umewakutanisha viongozi na wadau mbalimbali wa masuala ya lishe, wakiwemo Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Waganga Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri.

Mgeni Rasmi katika mkutano huo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe (Mb.).