Wilaya ya Mjini. 20.11.2026. Serikali inamatarajio makubwa kwa Jumuiya ya Maafisa habari na Mawasiliano, Mawasiliano na Uhusiano Zanzibar (ZICOO) katika kuielezea na kuitangaza miradi ya Serikali
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mattar Zahor Massoud ameyasema wakati wakati Viongozi wa Jumuiya ya ZICOO, walipofanya ziara Ofisini kwake Migombani Wilaya ya Mjini.
Amesema licha ya Serikali kulekeleza miradi mikubwa ya maendeleo bado taarifa za miradi hiyo hazijawafikia Wananchi ipasavyo.
Hivyo ni jukumu la ZICOO kuweka mpango maalum wa kuitembelea miradi hiyo na kupata taarifa sahihi kwa ajili ya kuwafikishia Wananchi ili kufahamu juhudi za Serikali yao.
Msaidizi na Mshauri wa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Bw. Mohammed Mansour amesema miradi ya kimkakati kama vile ya Uchumi wa Buluu, Utalii na Michezo, inapaswa kutangazwa ipasavyo ili jamii ipate uelewa wa kutosha.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maafisa habari, Mawasiliano na Uhusiano (ZICOO) Raya Hamad Suleiman amesema, vitengo vya habari vinahitaji kuwekewa Bajet maalum ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi.
Jumuiya ya Maafisa habari, Mawasilino na Uhusiano Zanzibar (ZICOO), inatarajia kufanya Mkutano mkuu visiwani Zanzibar tarehe 26/01/2027.
Imetolewa na Kitengo cha Habari, WHSUM.

