*Balozi Waziri aongoza ujumbe wa Wizara kwenye ushiriki wa mkutano huo;

*Makamu wa Rais atoa wito kwa Sekta za kimkakati za Viwanda na biashara, Nishati na kilimo kuungabisha nguvu kuchochea ukuaji uchumi;

*Mataifa takriban 200 yashiriki mkutano huo wakiwemo mawazifi qa madini;

Dar es salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Balozi Waziri Rajab Salum leo Novemba 19, 2026 ameshiriki kwenye ufunguzi rasmi wa mkutano wa kimataifa wa madini na uwekezaji unaoshirikisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya madini ndani na nje ya nchi.

Mkutano huo unaongozwa na kauli mbiu ‘’ Madini yaliyoongezwa thamani chachu ya kukuza sekta ya viwanda na ukuaji wa uchumi wa nchi, ina lengo la kuwakutanisha wadau ilu kujadili fursa za uwekezaji kwenye sekta ya madini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkutano huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Deogratius Ndejembi amesema, sekta ya madini inachangia takribani asilimia 10.3 ya pato la Taifa na kuzitaka sekta za viwanda na biashara, Nishati na kilimo kuunganisha nguvu ya pamoja na sekta ya madini kuinua uchumi wa nchi na kuongeza kipato cha mtu mmojammoja.

Aidha Mhe Ndejembi amewahakikishia wawekezaji kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na kuwataka kuhakikisha wale wote wenye leseni za uwekezaji kuhakikisha wanaendeleza shughuli za uwekezaji.

Mkutano huo unawashirikisha Mawaziri wa madini kutoka nchi za Mali, Burundi, DRC Congo, Ghana, Somalia, Saudi Arabia, Afghanstan, anbapo Jumla ya washiriki 200 kutoka nje ya nchii kiwemo Sweeden, Marekani, na South Afrika wanashiriki mkutano huo.