Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Clement Sangu akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM) Ashraf Hassan, Katika ofisi za IOM Jijini Dar es Salaam Novemba 19, 2026 baada ya mazungumzo ya ushirikiano kati ya serikali na IOM katika utekelezaji wa Ajenda ya Uhamaji salama wa Wafanyakazi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Clement Sangu (Katikati) ,Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM) Ashraf Hassan (Kulia), akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa IOM pamoja na viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano katika ofisi za IOM Jijini Dar es Salaam Novemba 19, 2026 baada ya mazungumzo ya ushirikiano kati ya serikali na IOM katika utekelezaji wa Ajenda ya Uhamaji salama wa Wafanyakazi.

…………

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Clement Sangu, Novemba 19, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM) Ashraf Hassan, na kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano katika kusimamia masuala ya uhamaji ili kulinda haki na ustawi wa wafanyakazi wahamaji katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mhe. Sangu amesisitiza umuhimu wa IOM kuendelea kutoa msaada wa kitaalamu na kifedha katika utekelezaji wa vipaumbele vya Jukwaa la Kikanda la Uhamaji Kazi (RMFM), ambalo Tanzania inaliongoza kwa kipindi cha mwaka 2026–2028.

Ameeleza kuwa, Tanzania inalenga kuimarisha mifumo ya ulinzi wa wafanyakazi wahamaji, kuboresha utekelezaji wa mikataba ya ajira baina ya nchi, kurahisisha upatikanaji na ubadilishanaji wa takwimu za uhamaji kazi pamoja na kuweka mifumo madhubuti ya kurejea na kuwaunganisha tena wafanyakazi wahamaji katika shughuli za kiuchumi wanaporejea nchini mwao.

Amesisitiza pia umuhimu wa kuimarisha mifumo ya uratibu miongoni mwa nchi 11 wanachama wa RMFM na kuandaa Mkutano wa Nane wa Jukwaa hilo utakaofanyika Februari 2027 jijini Dar es Salaam, ukiwa na lengo la kuwasilisha hatua na matokeo yanayoonekana katika kuimarisha utawala wa uhamaji kazi kikanda.

Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano inaendelea kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi kuimarisha usimamizi wa masuala ya kazi, ajira na uhamaji nguvu kazi kwa manufaa ya wafanyakazi na maendeleo ya Taifa.

MWISHO.

Caption:

1. MGL9775.jpg ; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Clement Sangu akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM) Ashraf Hassan, Katika ofisi za IOM Jijini Dar es Salaam Novemba 19, 2026 baada ya mazungumzo ya ushirikiano kati ya serikali na IOM katika utekelezaji wa Ajenda ya Uhamaji salama wa Wafanyakazi.

2.MGL9784.jpg; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Clement Sangu (Katikati) ,Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM) Ashraf Hassan

(Kulia), akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa IOM pamoja na viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano katika ofisi za IOM Jijini Dar es Salaam Novemba 19, 2026 baada ya mazungumzo ya ushirikiano kati ya serikali na IOM katika utekelezaji wa Ajenda ya Uhamaji salama wa Wafanyakazi.