Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, anamwakilisha Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania (TMIC 2026). Mkutano huo unafanyika kuanzia tarehe 19 hadi 21 Novemba 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo unawakutanisha zaidi ya wadau 1,700 kutoka ndani na nje ya nchi kujadili namna ya kuongeza uchakataji wa madini nchini ili kukuza viwanda, kuongeza ajira na mapato ya Taifa.

Wizara ya Madini imeandaa mkutano huo kwa kushirikiana na Chemba ya Migodi Tanzania. Washiriki ni pamoja na viongozi na wawakiishi kutoka nchi mbalimbali za Afrika, kampuni za madini, wawekezaji, taasisi za fedha na watoa huduma za teknolojia. Majadiliano yanahusu fursa za uwekezaji katika dhahabu, kinywe, nikeli, shaba, madini adimu na niobiamu, pamoja na namna ya kuongeza ushiriki wa wachimbaji wadogo na kampuni za Kitanzania katika mnyororo wa thamani wa madini.