Na Hellen Mtereko,

Mwanza

Jeshi la Polisi Mkoa wa limefanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa 63 wanaojihusisha na makosa mbalimbali ya jinai, ikiwemo ya kujihusisha na dawa za kulevya,wizi na uvunjaji wa nyumba usiku,kupatikana na pombe ya moshi na mitambo ya kupikia pombe hizo.

Hayo yamebainishwa Novemba 18, 2026 na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa wakati alipokuwa akitoa taarifa ya matukio hayo kwa waandishi wa habari.

Amesema katika oparesheni iliyoanza Novemba 01 hadi 17 2026 zimekamatwa mali mbalimbali zikiwemo dawa za kulevya kilo 2 na gramu 6300,pombe ya moshi lita 28,redio 7,friji 6,majokofu 5,vin’gamuzi 3,spika 2,skrini za kompyuta 2,jiko la umeme 1,pasi ya umeme 1,feni 3,majiko ya gesi 2,televisheni 23,pikipiki 2,simu janja 17,magodoro 7,redio aina ya sabufa 7,viti vya plastiki 9,kibodi za kompyuta 10,injini za boti 3,nyavu za kuvulia samaki 100 na  

PlayStation 4, ambapo baadhi ya mali hizo tayari zimetambuliwa na kurejeshwa kwa wamiliki walioibiwa.

Aidha, amesema katika kuelimisha na kudhibiti matendo hatarishi ya usalama barabarani wameendelea kuimarisha misako na ukaguzi wa vyombo vya moto katika barabara kuu za kuingia na kutoka Jiji la mwanza na maeneo mbalimbali ya katikati ya mji ambapo jumla ya makosa hatarshi 1760 yamekamatwa na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

“Makosa hayo ni pamoja na ubovu wa vyombo vya moto, kuendesha kwa mwendokasi, kuyapita magari mengine sehemu zisizoruhusiwa, kuendesha akiwa amelewa, kuzidisha abria, kutokuvaa kofia ngumu, kushindwa kuheshimu ishara za barabarani na kutokusimama kwenye vivuko vya watembea kwa miguu”, Amesema Kamanda Mutafungwa

Amesema jumla ya madereva watatu wamefungiwa leseni kwakipindi cha miezi mitatu kwakosa la kuendesha gari wakiwa wamelewa ambao ni Hasani Mrisho Iddy (37) akiendesha gari na T 234 DBDToyota,Frank Godifrey Kali (43) akiendesha gari namba T 402 BDL Carina

Hiece na Katema Malembeka Kayege (32) akiendesha gari T 218 BVZ aina ya Tata Bus.