
………..
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Salum Hamduni ametoa taarifa ya awali kuhusiana na tukio la Meli ya Mv. Mwanza kugonga mwamba katika Ziwa Victoria majira ya saa nne asubuhi.
Taaarifa hiyo ameitoa leo Novemba 18, 2026 wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Bandari ya Mwanza Kusini.
Hamduni ameeleza Kuwa Meli hiyo ilikuwa kwenye utaratibu wakawaida wa majaribio kwa ajili ya matayarisho ya kuanza safari zake.
“Meli ya Mv. Mwanza ilikuwa imepaki hapa Bandari ya Mwanza Kusini lakini kwa upande wa Serikali kupitia Shirika la Meli Tanzania (TASHICO) walikuwa wako kwenye maandalizi ya awali ya kuona namna ya kuanzisha safari za meli hiyo kwa bahati mbaya ndipo tukio hilo likatokea na mpaka sasa wataalamu wamefanya uchunguzi na meli yetu iko salama”, Amesema Hamduni
Aidha, amesema kuwa wameshafanya mawasiliano na Wizara ya Uchukuzi na maelekezo ya Serikali ni kufanya uchunguzi wakina kwa lengo la kujua sababu halisi pamoja na madhara ambayo yameweza kujitokeza.
“Meli hii imepaki hapa na iko salama lakini tunataka kujihakikishia usalama zaidi kwakufanya uchunguzi wa kitaalam,timu ya wataalamu itaundwa kwakushirikiana na Wizara pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama,mamlaka za Serikali na wataalam ili uchunguzi huo ufanyike”,
Ameeleza kuwa mara baada ya uchunguzi kukamilika Serikali kupitia Wizara husika na Mkoa watarudi kutoa taarifa ya kina kwa wananchi, huku akiongeza kuwa timu hiyo itafanya kazi ndani ya siku kumi na nne na majibu yatakuwa yamepatikana.
Ndani ya Meli hiyo kulikuwa na wataalamu wa Wizara ya Uchukuzi ambao kwa namna moja au nyingine wanahusika moja kwa moja na suala zima la uendeshaji na ushauri wa Shirika la TASHICO
