INaibu Waziri wa Fedha, Mhe. Handisi Mshamu Ali Munde (Mb) akipokelewa na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Mhe. Anne Semamba Makinda, alipowasili katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika. Wakishuhudiwa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Amina Msengwa(katikati), jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Handisi Mshamu Ali Munde (Mb) akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika ambapo alitoa wito wa matumizi ya takwimu sahihi katika kuelekeza uwekezaji wa sekta ya maji, kilimo na miundombinu, jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Handisi Mshamu Ali Munde (Mb) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yanayoongozwa na kaulimbiu isemayo: “Kuweka Mifumo Rasmi ya Takwimu za Maji na Usafi wa Mazingira kwa Maendeleo Endelevu yanayostahimili Mabadiliko ya Tabianchi Barani Afrika”, jijini Dodoma.
PIX 4.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Handisi Mshamu Ali Munde (Mb) akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, nakala za Ripoti ya Kutathmini Upatikanaji Endelevu wa Huduma za Maji, Vyoo na Usafi wa Mazingira, katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika iliyofanyika jijini Dodoma.
PIX 5.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Elke Wisch, akizungumzia namna Shirika hilo linavyoshirikiana na Serikali katika kuleta maendelo ya jamii, katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika iliyofanyika jijini Dodoma.
PIX 6.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali, kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Amina Msengwa akinzungumzia jitihada mbalimbali zilizofanywa na taasisi hiyo kuhakikisha takwimu rasmi zinapatika kwa ajili ya kupanga maendeleo nchini, katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika iliyofanyika jijini Dodoma.
PIX 7.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Handisi Mshamu Ali Munde (Mb) akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, nakala za Ripoti ya Kutathmini Upatikanaji Endelevu wa Huduma za Maji, Vyoo na Usafi wa Mazingira, katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika, iliyofanyika jijini Dodoma.
PIX 8.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Handisi Mshamu Ali Munde (Mb), akiwakabidhi washindi wa kwanza wa Mashindano ya NBS Data Challenge mfano wa hundi wenye thamani ya sh. Milioni 20, katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika, iliyofanyika jijini Dodoma.
PIX 9.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Handisi Mshamu Ali Munde (Mb), akimkabidhi tuzo mwanafuzi aliefanya vizuri katika masomo ya takwimu kwenye ngazi ya Shahada ya Uzamili kutoka Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Bi. Ester Joseph, katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika, iliyofanyika jijini Dodoma.
PIX 10.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Handisi Mshamu Ali Munde (Mb) akisindikizwa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Amina Msengwa, baada ya kumaliza hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika, iliyofanyika jijini Dodoma.
PIX 11.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Handisi Mshamu Ali Munde (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wanafuzi waliofanya vizuri katika masomo ya takwimu katika ngazi za Shahada ya Uzamili, Shahada, Stashahada na Astashahada kutoka Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika, iliyofanyika jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Dodoma)
…………….
Na. Josephine Majura na Farida Ramadhan, WF, Dodoma
Serikali imetoa wito wa matumizi ya takwimu sahihi katika kuelekeza uwekezaji wa sekta ya maji, kilimo na miundombinu ili kuongeza uzalishaji, kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.
Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika.
Mhe. Munde alisema kuwa takwimu ni nyenzo muhimu katika kubaini mahitaji ya wananchi, kupanga matumizi ya rasilimali na kuhakikisha uwekezaji unaleta matokeo yaliyokusudiwa.
“Maji ni rasilimali yenye mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi, hususan katika uzalishaji wa chakula, kilimo, viwanda, afya na uhifadhi wa mazingira, hivyo ni muhimu kuwa na mifumo imara ya takwimu ili kusimamia rasilimali hiyo kwa ufanisi”,alisema Mhe. Munde.
Alisema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuwekeza katika sekta ya maji kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa huduma hiyo na kutekeleza azma ya kumtua mama ndoo kichwani, hatua inayolenga kuwawezesha wanawake na watoto kutumia muda wao katika shughuli za uzalishaji na masomo badala ya kutafuta maji.
Mhe. Munde alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Maji na Mamlaka za Maji kwa mwaka 2025/26, upatikanaji wa huduma ya maji umefikia wastani wa asilimia 85.2 vijijini na asilimia 92.5 mijini, ambapo Serikali imepanga kukamilisha takriban miradi 1,214 ya maji, ikiwemo miradi 992 vijijini, 196 mijini na Miradi 26 ya Usafi na Mazingira maeneo ya mijini katika mwaka wa fedha 2026/27.
“Maji tuliyonayo hayapaswi kutazamwa kama hitaji la matumizi ya nyumbani pekee, bali pia kama rasilimali muhimu kwa uzalishaji wa chakula, maendeleo ya kiuchumi, uhifadhi wa mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi”, alisisitiza Mhe. Munde.
Alisema Serikali imeendelea kutekeleza miradi ya ujenzi, ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya umwagiliaji ili kupunguza utegemezi wa mvua, kuongeza uzalishaji wa chakula na kuimarisha kipato cha wakulima hatua iliyowezesha eneo linalomwagiliwa kuongezeka kutoka hekta 727,280.06 mwaka 2024/25 hadi hekta 983,466.60 mwaka 2025/26.
Alibainisha kuwa uwekezaji huo ni muhimu katika kuongeza uzalishaji wa chakula, kuimarisha usalama wa chakula nchini na kuongeza kipato cha wakulima, huku takwimu zikisaidia kubaini maeneo yenye uhitaji mkubwa wa miundombinu hiyo.
Mhe. Munde alisema kuwa mabadiliko ya tabianchi, yakiwemo ukame na mafuriko, yanaendelea kuwa changamoto katika upatikanaji wa maji na uzalishaji wa kilimo, hivyo kuna umuhimu wa kuimarisha mifumo ya takwimu ili kufanya maamuzi yanayozingatia hali halisi ya rasilimali zilizopo.
Aidha, amezitaka Wizara, mamlaka za maji, mikoa na halmashauri kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) katika kuimarisha ubora, uratibu na upatikanaji wa takwimu kwa wakati, akisisitiza kuwa machapisho yaliyozinduliwa yanapaswa kutumika katika maamuzi na utekelezaji wa mipango ya maendeleo.
Pia, amewahimiza wananchi kuendelea kutoa taarifa sahihi wakati wa sensa na tafiti mbalimbali ili kuiwezesha Serikali kupata takwimu zinazowakilisha mahitaji halisi ya wananchi.
Awali akizungumzia takwimu katika Sekta ya Maji, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri alisema matumizi ya taarifa sahihi na zinazopatikana kwa wakati ni muhimu katika kubaini maeneo yenye upungufu wa huduma na kuelekeza uwekezaji kulingana na mahitaji halisi ya wananchi.
Alisema kwa mujibu wa takwimu za sekta ya maji, Tanzania ina jumla ya vijiji 12,333, ambapo vijiji 10,758 vimefikiwa na huduma ya maji safi na salama, huku vijiji 1,575 vikiwa bado havijafikiwa, kutokana na hali hiyo, Serikali imepanga kuanza kutekeleza miradi ya maji katika vijiji 400, hatua inayodhihirisha umuhimu wa takwimu katika kupanga vipaumbele na kugawa rasilimali.
Mhandisi Mwajuma alisema pamoja na takwimu zinazoonesha kiwango cha upatikanaji wa huduma za maji, ni muhimu kuimarisha ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa kuhusu hali ya vyanzo vya maji, mwenendo wa mvua, mtiririko wa mito, kiasi na ubora wa maji pamoja na utendaji wa miundombinu.
Alieleza kuwa taarifa hizo zitasaidia kutambua mapema athari za ukame na mafuriko, kutabiri changamoto zinazoweza kujitokeza na kuwezesha uwekezaji katika miundombinu inayostahimili mabadiliko ya tabianchi.
Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali, kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Dkt. Amina Msengwa alisema inaendelea kuimarisha matumizi ya teknolojia za kisasa katika uzalishaji na uchambuzi wa takwimu ili kuongeza ufanisi wa maamuzi ya Serikali na sekta binafsi.
Alisema kupitia Mpango Kabambe wa Pili wa Takwimu Tanzania (TSMP II), wataalamu 79 wamewezeshwa kitaaluma na taasisi 27 zimeunganishwa katika Mfumo Jumuishi wa Takwimu Tanzania (TISP), hatua inayolenga kurahisisha upatikanaji na matumizi ya taarifa kutoka vyanzo mbalimbali kwa ajili ya mipango ya maendeleo na uwekezaji.
Aliongeza kuwa NBS pia imeanza kuweka kipaumbele katika kuanzisha Maabara ya Uchambuzi wa Data (Data Analytics Laboratory), itakayowezesha kuunganisha na kuchambua taarifa zinazotokana na sensa, tafiti, takwimu za kiutawala na vyanzo vipya kwa kutumia Akili Unde (AI) na teknolojia za kijiografia.
“Maabara itawezesha kuunganisha na kuchambua data za sensa, tafiti, takwimu za kiutawala na vyanzo vipya, kwa kutumia akili unde, uchambuzi wa kijiografia na makadirio ya maeneo madogo. Itasaidia kutoa taarifa za kina kwa wakati, kupima mbinu mpya kabla ya matumizi rasmi na kutoa mafunzo ya vitendo kwa wataalamu na vijana” alibainisha Dkt. Msengwa.
Aidha, Dkt. Msengwa amesema NBS inaendelea kukuza ushiriki wa vijana katika sekta ya takwimu kupitia programu za ubunifu na mashindano ya NBS Data Challenge, yaliyolenga kutumia teknolojia na uchambuzi wa data kutafuta suluhisho la changamoto mbalimbali za maendeleo.
Katika maadhimisho hayo, Serikali imezindua machapisho manne ya takwimu yatakayosaidia kuboresha mipango ya maendeleo na uwekezaji nchini. Machapisho hayo ni Wasifu wa Kiuchumi na Kijamii wa Mikoa, Mkakati wa Taifa wa Kuendeleza Takwimu wa mwaka 2026/27 hadi 2036/37, Mwongozo wa Ukusanyaji wa Viashiriavya Takwimu za Maji, Vyoo na Usafi wa Mazingira wa mwaka 2025/26 na Ripoti yaKutathmini Upatikanaji Endelevu wa Huduma za Maji, Vyoo na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2023.
Siku ya Takwimu Afrika huadhimishwa kila mwaka Novemba 18 tangu mwaka 1990 kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya takwimu katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kimazingira. Kwa mwaka 2026, maadhimisho hayo yanaongozwa nakaulimbiu isemayo: “Kuweka Mifumo Rasmi ya Takwimu za Maji na Usafi waMazingira kwa Maendeleo Endelevu yanayostahimili Mabadiliko ya Tabianchi Barani Afrika.”
