Na WMJJWM – Dodoma 

Kamishna msaidizi wa Ustawi wa jami kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Wakili Happy Msimbe amewasihi wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma kujiepusha na matumizi yaisiyo sahihi ya mitandao ili kulinda maadili na utu wao. 

Amesema hayo mara baada ya ibada ya misa ya jumapili iiliyofanyika tarehe 15 Novemba 2026, chuoni hapo ikiambatana na semina kwa wanafunzi hao iliyolenga kuwapa elimu wanafunzi kwa kulinda maadili, kujiepusha na matumizi yasiyo sahihi ya mitandao ya kijamii na kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

“Nawaomba sana mzingatie maadili mema, mana ninnyi ni wazazi wa kesho, hivyo mnatakiwa kuwa mfano bora kwa jamii na Taifa”amesema Kamishna Happy

kwa upande wake Msaikolojia kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Tito Lulandala amesema kuwa ili wanafunzi wafanikiwe katika maisha yao ni lazima kuamua kuishia masisha yenye misingi ya maadili, kujituma na kuchagua marafiki sahihi. 

“Naomba mfahamu kwamba kesho yako inaamuliwa na maamuzi na uchaguzi utakaofanya leo, hivyo jifunze maarifa mbalimbali Kadiri uwezavyo ili kuwa na hazina ya uwezo wa kitaaluma na ujuzi utakaokusaidia kutatua chagamoto mbalimbali za kijamii.” amesema Lulandali.

Naye Meneja wa Makao ya watoto ya Taifa Kikombo Darius Kalijongo amewahimiza wanafunzi kuepuka kufanya vitendo vya ukatili wa kimwili, kihisia na kiuchumi kwa sababu vitendo hivyo huathiri mafanikio ya kimasomo na maendeleo binafsi.

Mafunzo hayo yametolewa kwa wanafunzi wa ndaki ya elimu na tiba katika chuo kikuu cha Dodoma yanalenga kuwajenga wanafunzi kuwa na maadili mema, nidhamu, malezi na makuzi na kuwaandaa kuwa viongozi bora kuanzia katika familia, jamii na Taifa.