Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, leo tarehe 14 Novemba 2026 amenza ziara ya kikazi mkoani Lindi kwa kuzungumza na wananchi wa Madangwa, Jimbo la Mtama ukiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi katika mikoa ya kusini.
Madangwa ni kituo cha kwanza cha Mhe. Ndejembi akitokea mkoani Mtwara. Akiwasili katika eneo hilo Makamu wa Rais amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Adam Malima, Mbunge wa Mtama Mhe. Nape Nnauye, Wabunge wa Mkoa wa Lindi, pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali.
Akiwa katika eneo hilo, Makamu wa Rais ameilekeza Wizara ya Ujenzi kuanza kulipa fidia ikiwezekana kwa awamu kwa wananchi waliopisha ujenzi wa barabara katika eneo hilo.
Pia, katika ziara hiyo eneo la Madangwa, Wizara ya Maji imeahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni mia tano ili kuweza kukarabati mradi wa maji na huduma hiyo kuweza kupatikana ndani ya miezi miwili. Halikadhalika Wizara ya Kilimo imeahidi salfa ya unga kwaajili ya zao la korosho itawafikia wakulima kabla ya mwezi machi 2027.
Makamu wa Rais, alianza ziara ya siku Saba mikoa ya kusini iliyoanza tarehe 09 Novemba 2027, kwa kutembelea mkoa wa Ruvuma, Mtwara na sasa Lindi akikagua miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.

