Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Fatma Abdallah (katikati), akikata utepe kuzindua rasmi mgahawa wa Hungry Lion katika kituo cha Puma Energy Oysterbay, jijini Dar es Salaam, Novemba 13, 2026. Ushirikiano huo unaimarisha nafasi ya Puma Energy kama kampuni inayotoa huduma zaidi ya mafuta, huku ukiboresha uzoefu wa wateja, kuvutia uwekezaji na kuongeza fursa za ajira nchini. Wanaoshuhudia uzinduzi huo ni pamoja na Mkuu wa Hungry Lion Tanzania, Gladstone Okumu (wa pili kulia), Katibu wa Pili wa Masuala ya Siasa katika Ubalozi wa Afrika Kusini, Ndumiso Mngadi (wa kwanza kulia), pamoja na viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo.

…………. 

DAR ES SALAAM, 13 Novemba 2026

Puma Energy Tanzania imezindua rasmi mgahawa wa Hungry Lion katika kituo chake cha Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo unaashiria kuanza kwa shughuli za Hungry Lion nchini Tanzania na kuingia kwa kampuni hiyo katika soko la Afrika Mashariki kwa mara ya kwanza. 

Tanzania inakuwa nchi ya nne ambayo Hungry Lion inafanya kazi na Puma Energy, baada ya Namibia, Zambia na Botswana. Ushirikiano huo ni sehemu ya mpango wa Hungry Lion wa kupanua biashara zake katika nchi mbalimbali za Afrika ambapo kampuni hiyo pia inatarajia kuingia Zimbabwe na Eswatini mwaka 2027. 

Kuanzishwa kwa huduma za Hungry Lion katika kituo cha Puma Energy Oysterbay kunaongeza wigo wa huduma kwa wateja wanaotembelea kituo hicho, huku kukiimarisha huduma zinazotolewa na Puma Energy nje ya biashara yake kuu ya mafuta. Hatua hiyo pia inaonesha namna kampuni inavyoendelea kuwekeza katika kuboresha vituo vyake na kuongeza huduma zinazokidhi mahitaji ya kila siku wateja wake. 

Katika maandalizi ya uzinduzi huo, Puma Energy iliboresha kituo chake cha Oysterbay na kukiandaa kwa ajili ya huduma za Hungry Lion.  

Uwekezaji huo unaonesha imani ya kampuni katika fursa za kiuchumi zilizopo nchini na dhamira yake ya kuendelea kupanua huduma zake Tanzania lakini pia utachangia upatikanaji wa ajira kupitia shughuli za ujenzi na maandalizi ya mgahawa huo, pamoja na ajira nyingine zinazotokana na uendeshaji wake. 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Bi. Fatma Abdallah, alisema ushirikiano huo unaakisi dhamira ya kampuni ya kuboresha vituo vyake na kuvifanya kuwa maeneo yanayowapatia wateja huduma mbalimbali zaidi ya zile za kawaida za mafuta.  

“Biashara yetu kuu ni mafuta, lakini tunatambua kuwa mahitaji ya wateja yanaenda zaidi ya hapo. Ndiyo maana tunaendelea kuwekeza katika huduma zinazorahisisha maisha yao ya kila siku na kuchangia maendeleo ya uchumi wa Tanzania. Kuanzishwa kwa Hungry Lion katika kituo chetu cha Oysterbay ni hatua nyingine katika juhudi hizo, kwani sasa wateja wetu wanaweza kupata huduma za chakula wanapotembelea kituo hicho,” 

“Mkakati wetu ni kuboresha vituo vyetu ili wateja waweze kupata huduma mbalimbali wanazohitaji katika eneo moja. Wanaweza kujaza mafuta, kununua vilainishi vya magari, kufanya manunuzi katika maduka yetu ya Shop Express, kupata huduma za kifedha kupitia ATM na mawakala wa huduma za kifedha, na sasa pia kupata chakula bora kupitia Hungry Lion. Hivi ndivyo tunavyotekeleza dhamira yetu ya kutoa huduma zinazokwenda zaidi ya mafuta,” alisema. 

Bi. Fatma alisema Puma Energy Tanzania itaendelea kuwekeza katika kupanua na kuboresha mtandao wake wa vituo vya huduma, ambao kwa sasa una zaidi ya vituo 105 vya mafuta nchini. 

Mbali na mtandao wake wa vituo vya huduma, Puma Energy Tanzania inaendelea kuwekeza katika suluhisho za nishati mbadala, zikiwemo Gesi Asilia Iliyoshindiliwa (CNG) na Gesi ya Petroli Iliyoyeyushwa (LPG). Kampuni pia inaendelea kuboresha miundombinu ya vituo vyake na kuanzisha huduma zinazolenga kurahisisha maisha ya wateja, zikiwemo maduka ya Shop Express na programu ya kidijitali ya Puma PRIS, inayowazawadia wateja wanapotumia bidhaa na huduma za kampuni. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Hungry Lion, Adrian Basson, alisema hatua za kampuni kuendelea wekeza na kupanua shughuli zake katika masoko mbalimbali barani Afrika zinaenda sambamba na dhamira yake ya kuongeza ajira na kuchangia ukuaji wa uchumi barani humo. 

“Ukuaji wa biashara una maana zaidi pale unapozalisha ajira. Ndiyo maana tunazingatia upanuzi endelevu wa biashara yetu. Kila mgahawa mpya tunaofungua unatoa nafasi ya kuajiri watu zaidi, kukuza vipaji vya ndani na kuchangia maendeleo ya jamii tunakofanyia kazi. Tunataka kujenga biashara imara ya Kiafrika ambayo, pamoja na kuwafikishia wateja bidhaa zetu, inatoa fursa za kiuchumi katika maeneo tunayofanyia kazi,” alisema. 

“Tanzania ni soko lenye fursa nzuri kwetu na tunafurahi kuanza safari yetu katika Afrika Mashariki kupitia nchi hii. Ushirikiano wetu na Puma Energy unatupa nafasi nzuri ya kukuza biashara yetu, na tunatarajia kuwa sehemu ya maendeleo ya uchumi wa Tanzania,” alisema. 

Uzinduzi huu unaonesha namna ushirikiano wa kimkakati kati ya kampuni za kimataifa na biashara zilizoimarika nchini unavyoweza kusaidia kuvutia uwekezaji, kuongeza ajira na kuanzisha huduma mpya zinazoboresha uzoefu wa wateja.