Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb), akizungumza katika Mahafali ya Ishirini na Nne ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida, yaliyofanyika katika viwanja vya TIA, mkoani Singida.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb), akimkabidhi zawadi mhitimu wa shahada ya pili ya uhasibu aliyefanya vizuri, Diana Kisaka, katika mahafali ya ishirini na nne ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida, yaliyofanyika katika viwanja vya TIA, mkoani Singida. 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Profesa William  Pallangyo, akizungumza wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya chuo, katika mahafali ya ishirini na nne ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida, yaliyofanyika katika viwanja vya TIA, mkoani Singida. 

Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara , Taasisi ya Uhasibu Tanzania Ndugu William Makoresho, akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi kufungua mahafali ya ishirini na nne ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida, yaliyofanyika katika viwanja vya TIA, mkoani Singida. 

PIX 5

Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Kampasi ya Singida, Dkt.James Mrema, akizungumza katika mahafali ya ishirini na nne ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida, yaliyofanyika katika viwanja vya TIA, mkoani Singida.

PIX 6

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb), (Katikati), akiongoza maandamano ya mahafali ya ishirini na nne ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida katika viwanja vya TIA, Mkoani Singida. kushoto ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara, Taasisi ya Uhasibu Tanzania Ndugu William Makoresho na kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Prof. William Pallangyo.

PIX 7

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb), akiwatunuku ngazi mbalimbali ya cheti wahitimu katika mahafali ya ishirini na nne ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida katika viwanja vya TIA, mkoani Singida.

PIX 8

Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhe. Godwin Gondwe, akizungumza na wahitimu katika Mahafali ya Ishirini na nne ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida katika viwanja vya TIA, mkoani Singida.

PIX 9

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb), akitembelea Mradi wa  ujenzi wa jengo la taaluma kujionea hatua iliyofikiwa katika ujenzi, alipofika chuoni hapo kwa ajili ya mahafali ya ishirini na nne ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida, yaliyofanyika katika viwanja vya TIA, mkoani Singida.

PIX 10

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb), akitembelea maonesho ya shughuli za ujasiriamali zinazotekelezwa na wanafunzi, alipofika chuoni hapo kwa ajili ya mahafali ya ishirini na nne ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida, yaliyofanyika katika viwanja vya TIA, mkoani Singida.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Singida)

…………….

Na. Scola Malinga na Abdul Madenge, WF, Singida.Serikali imesema itaendelea kuimarisha sekta ya elimu nchini kwa kuhakikisha kila mtoto anasoma kwa miaka kumi katika shule za Serikali bila kulipa ada, sambamba na kuimarisha elimu ya amali ili kuwajengea vijana ujuzi wa kujiajiri na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa.

Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Deogratius Luswetula (Mb), wakati akizungumza katika mahafali ya ishirini na nne ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida, yaliyofanyika katika viwanja vya TIA, mkoani humo.

Mhe. Luswetula alisema hatua hiyo inalenga kuhakikisha kila kijana anahitimu akiwa na maarifa na ujuzi utakaomwezesha kuendelea na elimu ya juu, kupata ajira au kujiajiri.

‘‘Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, Toleo la 2023, imeweka msingi wa mageuzi ya elimu yanayolenga kuandaa wahitimu wenye uwezo wa kukabiliana na mahitaji ya soko la ajira na kuchangia kufikia uchumi wa kipato cha kati cha juu’’, alisema Mhe. Luswetula.

Alisema katika hatua ya elimu ya juu, Serikali imeweka mikakati mitatu muhimu inayohusisha maboresho ya mitaala ili iendane na mahitaji ya soko la ajira, uwekezaji katika miundombinu ya kufundishia na kujifunzia pamoja na matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika ufundishaji, tafiti na utoaji wa huduma.

Mhe. Luswetula alisema Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) ni mfano wa uwekezaji unaolenga kuboresha mazingira ya vyuo vikuu, ikiwemo Kampasi ya Singida.

Aidha, Mhe. Luswetula aliwapongeza vijana wanaotumia teknolojia kimkakati kubuni fursa za maendeleo, ikiwemo vijana wa TIA kampasi ya Singida walioshiriki na kushinda mashindano ya mawazo ya biashara na kupata nafasi za kwenda kujifunza na kushindana katika nchi za Uganda, Kenya, Afrika Kusini na Urusi .

‘‘ Mafanikio ya vijana hao yanaakisi matarajio ya Dira 2050, inayolenga kujenga Taifa lenye vijana wenye maarifa, ujuzi na uwezo wa kujiajiri. Kwa mujibu wa mwelekeo huo, elimu inapaswa kuwa nyenzo ya kuwawezesha vijana kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao na kushiriki katika kujenga uchumi imara na shindani’’, alisema Mhe. Luswetula.

Aliwaasa wahitimu kutumia teknolojia kwa ajili ya kutengeneza kipato, kukuza biashara na kuwafikia wateja badala ya kuitumia katika udanganyifu, utapeli na kusambaza taarifa za uongo.

‘‘Pia, ninawahimiza kuzingatia uwajibikaji katika taaluma zenu, kulipa kodi kwa hiari na kudai risiti halali mnapofanya manunuzi, mkitambua mchango wa kodi katika kugharamia huduma za maendeleo nchini,’’alisisitiza Mhe. Luswetula.

Aidha, aliwahimiza wahitimu walionufaika na mikopo ya elimu ya juu kuanza kurejesha mikopo wanapoanza kupata kipato ili kuwawezesha Watanzania wengine kupata fursa ya elimu ya juu nchini.

Mhe. Luswetula alitoa rai kwa wahitimu kutumia maarifa na ujuzi walioupata kuanzisha miradi itakayowawezesha kujipatia kipato na kuchangia maendeleo ya jamii zao ikiwa ni pamoja na kutumia fursa za kiuchumi zilizopo katika Mkoa wa Singida kuanzisha shughuli za uzalishaji mali kutokana na fursa zilizopo katika kilimo cha alizeti, ufugaji, biashara na madini.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Profesa William Pallangyo, alisema Kampasi ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Singida wahitimu 1,656, wakiwemo wanawake 855 (asilimia 51.6) na wanaume 801 (asilimia 48.4) wametunukiwa ngazi mbalimbali na kipekee imeweka rekodi ya kwanza ya kuhusisha wahitimu wa shahada ya uzamili tangu kuanzishwa kwa kampasi hiyo mwaka 1974. 

Alisema mafanikio makubwa yameendelea kushuhudiwa katika uandikishaji wa wanafunzi wapya kwa mwaka wa masomo 2026/2027, ambapo tayari wanafunzi 1,631 wamesajiliwa huku idadi hiyo ikitarajiwa kufikia 1,750, ikichangiwa  na ongezeko la wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu ambapo wanafunzi 893 wa kampasi hiyo wamefanikiwa kupata zaidi ya shilingi milioni 696.

 

‘‘Katika kuboresha mazingira ya kujifunzia, Serikali ya Awamu ya Sita imefanya uwekezaji mkubwa wa kimkakati kupitia mradi wa HEET chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo ujenzi wa jengo jipya la taaluma umefikia asilimia 92 ambapo gharama ya mradi ni sh. bilioni 13.56, hivyo utakapokamilika utaongeza uwezo wa kampasi kuhudumia hadi wanafunzi 22,000 kutoka 2,600 wa sasa, huku ikitoa ajira za muda mfupi kwa wananchi 600 wa mkoani hapa,’’alisema Profesa Pallangyo.

Alisema mbali na taaluma, TIA Singida imejikita katika kutatua changamoto za kijamii kupitia tafiti 13 zilizofanywa ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa mkoa pamoja na kutoa mchango kwa jamii kupitia mkakati wa kuboresha ufaulu wa somo la hisabati katika Shule ya Sekondari  Mandewa, pamoja na ushiriki thabiti katika shughuli za michezo na maendeleo ya jamii.

Profesa Pallangyo alisema mafanikio hayo ni utekelezaji wa Dira 2050, inayosisitiza udahili wenye ubora unaoendana na soko la ajira, wahitimu wenye ujuzi wa vitendo na uwezo wa kujiajiri, pamoja na miundombinu ya kisasa ya kufundishia na kujifunzia.

 

Naye Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara , Taasisi ya Uhasibu Tanzania Bw. William Makoresho, aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Wizara ya Fedha, kwa kuendelea kuikuza TIA, na kuahidi kuwa Bodi itaendelea kuishauri menejimenti, ili kuhakikisha TIA inaendelea kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Aliwaasa wahitimu kujenga uwezo wa kiuchumi kwa kujifunza  kutunza na kuendesha fedha, kujiwekea akiba, kufanya maamuzi ya busara kuhusu fedha pamoja na kuziona fursa za uzalishaji na uwekezaji zinazowazunguka ili  kujenga msingi thabiti wa maisha ya baadaye.