📌Watoto wamefunga shule salama, nataka Januari wawe salama”Â
Na WMJJWM, Tarime
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Edward Gowele amewakemea na kuwataka kuacha mara moja wananchi wa wilaya hiyo wanaoendekeza mila ya ukeketaji hasa kipindi hiki cha likizo ndefu ya mwaka.
Gowele ametoa agizo hilo Novemba 12, 2026 akiwa katika kata ya Nyakonga, kijiji cha Magoto, akihitimisha Kampeni ya kutoa elimu ya kutokomeza ukeketaji katika mkoa wa Mara, hasa kipindi hiki cha likizo ndefu.Â
“Nawaomba watoto waendelee kuwa salama kwa kipindi chote cha likizo, Kampeni hii hatuifungi, sisi tunaendelea, nawaagize Maafisa maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii kwapamoja kuendelea kutoa elimu na kuhakikisha watoto wanakuwa salama”
Amezidi kusisitiza kwamba, ukeketaji ni mila iliyopitwa na wakati ambapo ni ukatili kwa watoto, unaoleta madhara ikiwemo ndoa na mimba za utotoni, matatizo ya kisaikolojia, kutojiamini, kukatisha masomo na kuua ndoto zao.
Amewataka kila mmoja akemee kwa nguvu zote vitendo hivyo, wazazi wasiwalazimishe watoto kukeketa na vielevile ni kinyume na sheria za nchi, hivyo wakikamwatwa watachukuliwa hatua.
Kwa upande wake, mratibu wa Kampeni hiyo Dennis Mose amesema kampeni hiyo iliyoanza Novemba 02 -12, 2026, imeratibiwa na Wizara na Maendeleo ya Jamii(, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI pamoja na wadau, imefanyika katika wilaya za Serengeti, Rorya na Tarime kwa kufanya midahalo na jamii katika kata 8, vijiji 16 na kuwafikia wananchi takribani elfu 17.

