Na Mwandishi Wetu-Singida
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Bw. Salum Mnuna, amewataka watumishi wa Mamlaka hiyo kuhakikisha wanaendelea kuwa chachu ya matokeo chanya katika utendaji na utoaji za kiudhibiti.
Mnuna ametoa maelekezo hayo wakati akifungua kikao cha kwanza cha Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo, mjini Singida, leo 11 Novemba 2026.
Amesisitiza kuwa, ili kufanikisha dhima hiyo, EWURA imeweka mazingira wezeshi yanayovutia sekta binafsi kushiriki kutoa huduma zinazodhibitiwa, imeongeza hamasa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia, kuimarisha utendaji wa mamlaka za maji nchinj sanjari na utekelezaji wa mpango kabambe wa kitaifa wa nishati.
Aidha, ameeleza kuwa, EWURA tayari inatumia mbinu thabiti na zenye ufanisi zinazochagiza matumizi ya teknolojia katika utoaji huduma za kiudhibiti, uimarishaji wa mifumo ya kidijiti na kuendelea kulinda maslahi ya wawekezaji, watoa huduma, watumiaji.

