Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, leo tarehe 9 Novemba 2026 amewasili mkoani Ruvuma kuanza Ziara ya Kikazi katika mikoa ya Ruvuma, Mtwara, Lindi na Pwani. 

Katika uwanja wa ndege wa Songea, Makamu wa Rais amepokelewa na Viongozi wa Mkoa wa Ruvuma, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Brigedia Jenerali Ahmed Abbas, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Ruvuma Oddo Mwisho, Mawaziri, Naibu Mawaziri, Wakuu wa Wilaya, Viongozi wa Dini, Viongozi wa kimila, Wazee wa Mkoa wa Ruvuma pamoja na wananchi mbalimbali 

Katika ziara hiyo, Mhe. Ndejembi atazungumza na wananchi, atakagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.