Rais wa Mtandao wa Mameneja wa Rasilimaliwatu Katika Sekta ya Umma Barani Afrika (APS-HRMnet) Bw. Xavier Daudi amesema maandalizi ya Mkutano wa 11 wa APS-HRMnet 2026 utakaofanyika katika eneo la Hotel Verde, Zanzibar yamekamilika kwa asilimia 90.

Ameongeza kuwa, washiriki wa mkutano wamepata Mwamko mkubwa wa kushiriki kwa kuwa makadirio ya awali ilikuwa 800 lakini hadi sasa washiriki wapatao 1200 wamejiandikisha.

Mwamko huo ni kutokana na Mkutano kufanyika Tanzania hususani Zanzibar ambapo ni sehemu ya kitalii, salama, yenye watu wakarimu na inavutia na kiwango cha uzingatiaji wa kiplomasia kipo juu.

Aidha, amewataka washiriki wa ndani kuanza kufika Zanzibar kuchukua vifurushi (package) vyao vya Mkutano tarehe 8 wakati washiriki wa mkutano kutoka nje ya Tanzania watatakiwa kuchukua tarehe 9 Novemba, 2026 katika eneo la Mkutano (Hotel Verde).

Amesema hadi sasa Nchi za Afrika zaidi ya 20 zinaleta washiriki ikiwa ni pamoja na Mawaziri na Makatibu Wakuu wenye dhamana ya Utumishi wa Umma.