Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imemhukumu Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Upinzani CHADEMA, Tundu Lissu kifungo cha miaka minne gerezani baada ya kumkuta na hatia ya kosa la uchochezi.

Uamuzi huo umetolewa leo Novemba 6, 2026, na kuhitimisha kesi iliyodumu kwa takribani miezi 19 tangu kukamatwa kwake.

Lissu awali alishatkiwa kwa kosa la uhaini hata hivyo hii Leo hakukutwa na hatia ya kosa hilo kupitia kesi ya uhaini namba 000019605 ya mwaka 2025,

Lissu alikamatwa Aprili 9, 2025, mjini Mbinga, mkoani Ruvuma, muda mfupi baada ya kuhutubia mkutano wa CHADEMA uliokuwa sehemu ya kampeni ya chama hicho ya No Reforms, No Election. Siku iliyofuata, Aprili 10, alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, na kusomewa mashtaka ya uhaini.