
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili Bungeni Jijini Dodoma kushiriki Kumbukizi ya Miaka 10 ya Kifo cha Hayati Samwel Sitta, ambapo atazindua kitabu cha maisha na safari ya uongozi wake. Hayati Samwel Sitta alikuwa Mbunge na Spika Mstaafu na pia amewahi kushika nyadhifa nyingine katika Serikali kuanzia Awamu ya Kwanza ya Utawala.
